The House of Favourite Newspapers

Abramovich Anaumia kweli Kuiweka Sokoni Chelsea

0

MMILIKI wa Klabu ya Chelsea, Roman Abramovich anaumia kuiweka sokoni timu hiyo na hayo yameonekana kupitia waraka ambao ameuandika.

Alhamis mmiliki wa Chelsea alithibitisha kwamba anaiuza timu hiyo ambayo alianza kuimiliki 2003 na ni miongoni mwa timu bora zinazoshiriki Ligi Kuu England.

Katika waraka huo moja ya sehemu inasomeka namna hii: “Tafadhali najua kwamba hii kwangu ni ngumu na ni maamuzi magumu ambayo nimefanya na yananiumiza mimi nadhani pamoja na timu pia lakini kivyovyote vile najua kwamba haya ni kwa manufaa ya klabu.

“Nina matumaini kwamba nitaweza kutembelea Stamford Bridge mara ya mwisho kuweza kusema kwa heri kwa kila mmoja. Ninafurahi kuwa mmoja wa mafanikio ya Chelsea na ipo ndani ya moyo muda wote,”.

Leave A Reply