The House of Favourite Newspapers

Baba yamkuta kwa ubakaji ‘katoto’

MSALA mzito! Baba mmoja, Chuma Mwakawala (59), mkazi wa Kijiji cha Mapogolo Kata ya Chokaa Wilaya ya Chunya jijini hapa yamemkuta baada ya kutiwa mbaroni na Polisi kabla ya kufikishwa Mahakama ya Wilaya ya Chunya kwa tuhuma za ubakaji wa ‘katoto’ ambako ni denti wa darasa la kwanza.

 

Mwakawala alidaiwa kuhusika na tukio hilo lililojiri hivi karibuni dhidi ya denti huyo mwenye umri wa miaka 12 (jina linahifadhiwa).

Akisoma mashtaka mbele ya Hakimu Mfawidhi Wilaya ya Chunya, Osmund Ngatunga, Mwendesha Mashtaka, Frederick Ndosi alisema mtuhumiwa alitenda kosa hilo kwa nyakati tofauti kati ya Julai na Oktoba, mwaka huu.

 

Alisema kuwa, Mwakawala alidaiwa kumbaka mwanafunzi huyo mara sita kwa nyakati tofauti akiahidi kumpatia shilingi elfu mbili huku akimtishia maisha endapo atatoa siri hiyo.

Ndosi aliiambia mahakama kuwa kosa hilo ni kinyume cha sheria namba 130 (1)(2)(e) na 131(1) sura ya 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002.

 

Mshtakiwa huyo alikana kutenda kosa na dhamana ilikuwa wazi, lakini mtuhumiwa hakuwa na wadhamini. Hakimu Ngatunga aliiahirisha kesi hiyo hadi itakapotajwa tena ambapo mshitakiwa atasomewa maelezo ya awali hivyo baba huyo alirejeshwa rumande.

STORI: EZEKIEL KAMANGA, MBEYA

MAGUFULI AWAAPISHA MAWAZIRI WAPYA, ATOBOA SIRI YA KUWATUMBUA – VIDEO

Comments are closed.