The House of Favourite Newspapers

Waziri wa Nishati Avunja Bodi ya REA

WAZIRI wa Nishati Dk Medard Kalemani leo (Novemba 12.2018) amevunja Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Nishati Vijiji REA kutokana na kutoridhishwa na utendaji kazi wake.

 

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma, Dkt. Kalemani amesema; “Kwa mujibu wa mamlaka niliyopewa chini ya kifungu 9 (3)(b) cha sheria No. 8 ya nishati vijijini ya 2005 nimeamua kuivunja bodi kwa kutengua uteuzi wa mwenyejuti pamoja na wajumbe wa bodi ya wakurugenzi ya wakala wa nishati vijijini kuanzia leo tarehe 12 novemba 2018″amesema Kalemani.

 

Aidha amesema kuwa bodi nyingine itaundwa baadae kwa mujibu wa sheria ya nishati vijijini ya mwaka 2005. Bodi hiyo iliyokuwa ikiongozwa na mwenyekiti wake Gigion Kaunda imedumu kwa muda wa mwaka mmoja.

 

Wajumbe wa Bodi ambao wametenguliwa ni pamoja na Mhandisi Innoceent Lwogwa,Happiness Mhina,Stella Mandago, Scholastica Jullu,Amina Chinja,Teobard Sabi na Michael Nyagoga.

Comments are closed.