The House of Favourite Newspapers

Babu Tale Amjibu P Funk, Adai Afrika Nzima Inatambua Mchango wa WCB

0
Babu Tale akiwa na Staa wa Bongo Fleva Diamond Platnumz

SIKU chache baada ya Prodyuza mkongwe wa muziki nchini, P Funk ‘Majani’ kudai kuwa Lebo ya Muziki ya ya WCB inawanyonya wasanii wake jambo ambalo limeibua mtifuano katika mitandao ya kijamii, hatimaye Meneja wa Diamond Platnumz, Babu Tale naye ameibuka na kumjibu.

Tale amelazimika kumjibu P Funk baada ya kuulizwa na waandishi wa habari nini kauli yake kuhusiana na sakata hilo ambapo alianza kuwa kusema aachwe mkongwe huyo hakuna sababu ya kumjibu huku akiongeza kuwa WCB ni wafanyabiashara na wanapata pesa nyingi hivyo suala la mikataba ni lazima katika biashara.

“Kama mkongwe kasema si vizuri kubishana naye, acha aseme, namuheshimu sana P Funk, mwache. Mikataba ya WCB haipo kwenye maiki ama kamera. Ulishawahi kumuona mtu amebandika mikataba kwenye kamera au maiki? Heshima ya Majani kwenye hii industry ya muziki ni kubwa, basi tumwache.

“La ndani linabakia ndani, ukimwona mtu analitoa la ndani kuwa la nje hajafundwa huyo. Nina miaka mingi kwenye industry ya muziki, nazungumza ninachoikifahamu, lakini tunabadilisha kutoka kwenye muziki wa kawaida kuwa biashara.

“Lazima kuwe na mikataba na makubalianao na makubaliano ni ya ndani, unapoona mtu anasimama kuyachambua makubalianao, ana mashaka. Na ukiona mtu anachambua mkataba wa pande mbili ambao hahusiki kwa namna yoyote achana naye, muheshimu.

Prodyuza Mkongwe P Funk ‘Majani’

“Kuhusu Rayvanny, Harmonize, Mavoko kujitoa sisi hatuna la kusema, sisi ni wafanyabiashara kwa hiyo tunaruhusu mtu yeyote aseme anachoona. Afrika nzima inatambua mchango wa WCB.

“Usiwaache watu wakutoe kwenye reli yako, vision yetu ni kutoka kimataifa, ukiwaacha watu wakutoe kwenye reli halafu ukawafuata, unatoka kwenye kile am,bacho umekidhamiria, hatuko tayari.

“Hatuwezi kuvunjika moyo, sisi ni wafanyabiashara wa muziki na muziki unatulipa kwelikweli, hatuoni sababu ya kuacha. Unapofanya biashara inayolipa lazima kuwe na makelele.

“Ukimuona mtu anapiga kelele kwenye biashara ya mtu anayopiga pesa, ujue yeye kuna sehemu ana matatizo, usibishane naye, mheshimu. Ukiona mtu ananishana na na sisi mpe big-up,” amesema Tale.

Leave A Reply