The House of Favourite Newspapers

Christina Shusho: Maswali Yenu Nitayajibu Na Ukweli Utajulikana

0
Mtumishi wa Mungu na mwimbaji mahiri wa muziki wa injili, Christina Shusho.

Mtumishi wa Mungu na mwimbaji mahiri wa muziki wa injili, Christina Shusho amefunguka kupitia ukurasa wake wa instagram kuwa siku ya kuongea ikifika ntaongea yote kuhusu ndoa ili ukweli ujulikane badala ya watu kueneza habari ambazo hawana undani wake. Niwaombe uvumilivu swala hili linapo endelea kufanyiwa kazi ”

“Ndugu Zangu, Waandishi wa Habari mnaonitafuta na Mashabiki Kwa Ujumla Ningependa kuchukua nafasi hii kuweka baadhi ya mambo sawa.

1.Najua mna maswali mengi kutokana na interviews nilizo fanya mwaka 2020 na nyingine mwaka wa 2022.
Niseme tu maswali haya yote nitayajibu kikamilifu hivi punde na Ukweli utajulikana.

2.Watu wanao tumia jina langu au picha zangu kwenye online kueneza habari za upotofu na wengine kutukana:
Jambo hili liko kisheria na nina Imani Hatua stahiki zitachukuliwa kwani wanasheria na Mamlaka husika wana taarifa zote.

3.Siku ya Kuongea ikifika ntaongea yote kuhusu Ndoa ili Ukweli julikane badala ya watu kueneza habari ambazo hawana undani wake. Naamini Ukweli siku zote humuweka mtu huru. Niwaombe uvumilivu swala hili linapo endelea kufanyiwa kazi ” amesema Christina Shusho.

Leave A Reply