The House of Favourite Newspapers

BABU TALE ATOBOA SIRI YA KUMWACHA HAWA INDIA

MENEJA wa Kundi la Wasafi Classic Baby (WCB), Hamisi Taletale ‘Babu Tale’ ameibuka na kutoboa siri ya kumuacha nchini India alikompeleka hivi karibuni kwa ajili ya matibabu msanii wa Bongo Fleva, Hawa Mayoka ‘Hawa wa Nitarejea’.  

 

Akipiga stori na Star Showbiz, Babu Tale alisema amerejea nchini na kumuacha Hawa India kwa kuwa msanii huyo anaendelea vizuri hivyo baada ya kushauriana na madaktari wake walimwambia asiwe na wasiwasi mgonjwa yupo sehemu salama hakuna ulazima wa yeye kuendelea kumsimamia muda wote.

 

“Madaktari ndiyo walioniruhusu nirudi Bongo na wakanihakikishia hali ya mgonjwa wangu inaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo hivyo hakuna ulazima wa mimi kuendelea kuwepo muda wote kama nitahitajika kwa lolote watanijusha.

 

“Baada ya kupata kauli ya wataalamu hao nikaona nirudi nije kuendelea na mambo mengine huku nikiwasiliana nao kiukaribu zaidi,” alisema Babu Tale.

Hivi karibuni Mkurugenzi wa WCB ambaye ni mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ alijitolea kumpeleka Hawa nchini India kwa matibabu yatakayogharimu milioni 50 ya ugonjwa uliothibitishwa na madaktari hapa Bongo kuwa ni ini kuwa na tatizo lakini alipofika huko aligundulika kuwa ana tatizo la moyo na kufanyiwa upasuaji.

Comments are closed.