visa

Babu wa Miaka 78 Arejea kwa Mkewe Baada ya Miaka 26

MZEE Edward Mwangi (78) kutoka Gikangu kaunti ya Murang’a nchini Kenya aliondoka nyumbani kwake miaka 26 iliyopita baada ya kuzozana na mkewe, alikaa Nairobi kabla ya kwenda Nakuru ambako alikuwa akifanya kazi mashambani.

 

Mzee Mwangi aliondoka na redio na amerudi na redio ile ile huku akiwa amesahau nyumbani kwake. Aliamua kwenda kutafuta ajira baada ya kuona kuwa ndoa yake haiendi sawa.

 

Alirudi nyumbani kwake Februari 6, 2020 baada ya kupata msaaada kwa rafiki yake anayeitwa Weruweru Kamau, ambaye alimsaidia kwa kutafuta wa kumchangia pesa kwa ajili ya usafiri ili arejee kwake. Aliondoka bila kusema kama atarudi na nduguze walimtafuta bila mafanikio kwa miaka yote hiyo.
Toa comment