Baby J: Siumii kukwapuliwa bwana, mwanangu ananipa furaha

WANAOSEMAGA kidonda cha mapenzi hakiponi wako wapi? Baada ya kudaiwa kukwapuliwa bwana na dada wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond, Esma, mwanamuziki maarufu visiwani Zanzibar, Jamila Abdalah ‘Baby J’ amesema mwanaye aliyebaki naye anampa furaha.

 

Baby J aliyasema hayo akizungumza na Za Motomoto ya Risasi kuwa, siku zote kwenye maisha unapopatwa na jambo, usikubali kulibeba na kukufanya moyo wako ububujikwe damu na wakati waweza kuendelea na maisha yako.

“Mimi nakula bata na mwanangu uzuri ni kwamba sitaki hata siku moja kuumiza moyo wangu kwa muda mrefu, jambo muhimu kwangu ni vile ninavyomuona mwanangu ana amani na afya njema ndiyo kila kitu kwangu na si kingine,” alisema Baby J.


Loading...

Toa comment