The House of Favourite Newspapers

Bahati Bukuku akubali mumewe kuoa mke mwingine

DAR ES SALAAM: Muimbaji wa nyimbo za Injili, Bahati Bukuku ameridhia aliyekuwa mumewe Daniel Basila kuoa mwanamke mwingine kwani walishapeana talaka siku nyingi.

Bahati ameongea hayo baada ya kupata habari kuwa mumewe amepata mchumba anayeitwa Elizabeth Ngaiza na wanatarajia kufunga ndoa hivi karibuni.

 

“Unajua kwanza ndio nazipata habari hizi za mume wangu kuoa lakini sina kipingamizi kwani nilishaachana naye siku nyingi na alinipa talaka rasmi mahakamani Julai mwaka huu, hivyo sioni tatizo kabisa,” alisema Bahati.

 

Hata hivyo ndugu wa karibu na familia hiyo aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema kuwa, mume wa Bahati kwa sasa ameamua kuhama kabisa na kwenda kuchumbia mkoani kwani yeye na Bukuku walikaa mbali kwa miaka 14 ambapo kwenye ndoa yao walipata mtoto mmoja ambaye alifariki.

 

“Daniel na Bahati walikaa kwenye ndoa kwa muda mfupi sana, walitengana kwa miaka 14, kila mmoja akijua ipo siku watarudiana kwani walikuwa na ndoa ya kanisani lakini baada ya Daniel kushindwa kuvumilia, ameamua kumpa talaka mkewe na sasa ndio amechumbia ili aingie tena kwenye ndoa,” alisema ndugu huyo aliyeomba jina lake lisiandikwe gazetini.

 

Eliza na Daniel walikutana mkoani Dodoma ambapo walikuwa wameenda kutoa huduma kwani Eliza naye ni muimba Injili kama alivyo Bahati Bukuku.

“Wawili hao walivyokutana kwenye huduma walibadilishana namba za simu ambapo Eliza hakujua kuwa ni mtaliki wa Bukuku, wakaanzisha uhusiano uliozaa uchumba na sasa wanaelekea kwenye ndoa,” alisema ndugu huyo.

Stori: Neema Adrian, Amani

LIVE: WAZIRI MKUU akihairisha bunge leo Novemba 16, 2018

Comments are closed.