The House of Favourite Newspapers

Mama ampa masharti bwana wa Mobeto

DAR ES SALAAM: Msimamo! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya mama wa mwanamitindo maarufu Bongo, Hamisa Mobeto, Shufaa Rutiginga kuonesha msimamo wake na kumpa masharti ya kufanya bwana mpya wa bintiye, Josh Adeye ili aweze kumpitisha na kuwa mkwewe.

 

Mama huyo amefunguka hayo mara baada ya ‘mapichapicha’ kusambaa kwenye mitandao ya kijamii hususan Instagram yakimuonesha Mobeto akiwa na Josh ambaye ni staa wa mipira wa kikapu nchini Marekani.

Picha hizo ziliwaonesha wawili hao wakila bata kwenye viwanja mbalimbali nchini humo huku wafuasi wa mrembo huyo wakionesha kufurahishwa na uhusiano huo mpya baada ya mrembo huyo kumwagana na mzazai mwenzake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

 

Akizungumzia picha hizo, bi mkubwa huyo alisema, msimamo wake ni kwamba, hata kama picha hizo zinaonekana na yeye kuziona kwenye mitandao lakini bado anamtambua tu kama hawara.

Mama Mobeto alisema, kama kweli jamaa huyo anamhitaji mwanaye basi masharti anayompa ni kufika nyumbani kwanza nyumbani kwake kujitambulisha ili amjue vizuri yeye pamoja na ndugu zake.

Alisema akishamjua, atamuelekeza hatua ya kufuata na taratibu zote za kimila ili aweze kumuoa ili awe mume halali.

 

Alisema kama mzazi mwenye maadili, amekuwa akishindwa hata kumzungumzia mwanaume huyo hadi pale atakapojitambulisha rasmi nyumbani kwake.

“Hivi jamani umeona wapi mzazi ambaye anajua maadili amuongelee hawara wa mtoto wake ambaye hajatambulika rasmi? Aje nyumbani, ajitambulishe, hapo sasa nitakuwa free kumuongelea, lakini habari za kwenye mitandao siwezi kuzizungumzia,” alisema mama huyo.

 

Mbali na Amani, kabla ya bintiye huyo hajajianika kimahaba na jamaa huyo, bi mkubwa huyo alinukuliwa na gazeti dada na hili la Ijumaa Wikienda ambapo alisema hawezi kumzungumzia kabisa bwana huyo kwa kuwa hamtambui lakini kwa sasa ameamua kumpa masharti ili akiweza, achukue jiko mzima.

Stori: Imelda Mtema, Amani

Comments are closed.