The House of Favourite Newspapers

Balaa la Vanessa, Amtaja Jux Jukwani, Mashabiki Walipuka – Video

TAMASHA la Utamaduni linaloendelea jijini Dar es Salaam, Jama Festival, limezidi kunoga baada ya wasanii mbalimbali kuibuka na kulipamba tamasha hilo huku wakipanda stejini na kufanya maajabu ya burudani.

 

Usiku wa kuamkia leo ilikuwa zamu ya Malkia wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee  ‘Vee Money’ na Hamad Ally ‘Madee’ na Dogo Janja ambapo Vee Money alikuwa wa kwanza kupanda jukwaani, lakini cha kushangaza wakati akipafomu na alimtaja aliyewahi kuwa mpenzi wake, msanii JUX katikati ya mistari ya wimbo wake aliokuwa anaimba jambo lililoibua shangwe ya hatari kwa mashabiki waliokuwapo kwenye shoo hiyo.

 

Jama Festival ni tamasha lililoandaliwa na jumuiya ya Afrika Mashariki lenye lengo la kuonyesha utamaduni wa nchi hizo likihusisha nchi za Tanzania Kenya, Uganda, Sudan Kusini, Burundi na Rwanda na lilianza Septemba 21, litatamatika leo Septemba 28, 2019.

 

Comments are closed.