The House of Favourite Newspapers

RAIS wa Real Madrid Amuweka Sokoni Gareth Bale

RAIS wa Real Madrid, Florentino Perez ameamua kumweka sokoni winga wa timu yake, Gareth Bale. Uamuzi wa Perez umeshangaza wengi kwa kuwa kwa muda mrefu alikuwa hataki kumuuza akiamini kuwa ndio angeweza kuziba pengo la Cristiano Ronaldo.

 

Bale amekuwa analaumiwa kwa kucheza kiwango cha chini cha soka na pia kutokuwa na uhusiano mzuri na wenzake.

 

Pia hivi karibuni alituhumiwa na Shirikisho la Soka Hispania kwa kutoa ishara mbaya ya kuwakejeli mashabiki wa Atletico Madrid ilipocheza na Real Madrid.

 

“Bale kwa kweli hana muda mrefu katika timu ya Real Madrid kwa kuwa amemchosha Rais wa klabu,” alisema mtu wa karibu wa Perez. Wakati Ronaldo alipouzwa kujiunga na Juventus, Perez aliweka matumaini yake kwa Bale kuwa ndio atakuwa mkombozi wa timu hiyo.

 

Hata hivyo, Bale amekuwa na msimu mbovu, ambapo amepachika mabao 13 tu msimu.

 

Kufuatia hali hiyo, Bale amejikuta akiwekwa benchi na kocha wa Real Madrid, Santiago Solari. Inasemekana tangu ametua Real Madrid mwaka 2013, Bale amecheza asilimia 58% ya mechi za timu hiyo huku akipachika mabao 101. Tangu amejiunga na timu hiyo alipachika mabao mengi zaidi katika msimu wa 201314, ambapo alifunga mabao 22.
MADRID

Comments are closed.