Balinya Asisitiza Ndio Kazi Imeanza

Mganda Juma Balinya

BAADA ya kutupia mabao mawili kwenye mechi mbili za kirafiki, bunduki ya Yanga, Mganda Juma Balinya imefunguka.

 

Balinya amefunga mabao hayo mawili katika mechi za kirafiki ambazo Yanga wamezicheza mkoani Morogoro walipoweka kambi. Balinya alizifunga timu za Moro Kids na Tanzanite.

 

Kabla ya kujiunga na Yanga kwa msimu uliopita alifunga mabao 19 na kuwa Mfungaji Bora katika Ligi Kuu ya Uganda.

 

Straika huyo aliyesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo amesema uwezo huo aliounyesha katika mechi hizo ni mwanzo wa mambo makubwa atakayofanya klabuni hapo.

 

“Hapa ndiyo kazi imeanza, bado kuna vitu vingi ambavyo nitafanya katika timu kwa msimu ujao. Kitu kikubwa watu wasubiri.

 

“Nitapambana kuhakikisha naitimiza kazi yangu ya kufunga vile inavyotakiwa, kwa sababu hilo ni jukumu langu na lazima nilifanye,” alisema Balinya.


Loading...

Toa comment