The House of Favourite Newspapers

BALOZI WA CHINA AZINDUA UJENZI OFISI YA WALIMU MAKUMBUSHO  

Ofisa elimu wa  Mkoa wa Dar es Salaam akizungumza jambo kwenye hafla hiyo.
Balozi wa China nchini Tanzania,Wang Ke (katikati) akimwonyesha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda baadhi ya nyaraka zenye orodha ya vitu vitakavyotumika wakati wa ujenzi.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Makumbusho jijini Dar es Salaam wakiwa katika hafla hiyo ya uzinduzi wa ujenzi wa ofisi  za walimu.
Viongozi hao wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa ujenzi huo.

Baadhi ya wanafunzi wa Shule  ya Sekondari ya Makumbusho wakifuatilia kilichokuwa kikiendelea.
Baadhi ya walimu na wazazi waliohudhuria hafla hiyo.
Zoezi la kukata utepe likiendelea.

 

BALOZI wa China nchini Tanzania,  Wang Ke, leo amezindua ujenzi wa ofisi ya walimu katika shule ya sekondari ya Makumbusho na kuahidi kujenga ofisi nne za walimu  za Mkoa wa Dar es Salaam ili kusaidia  kuinua kiwango cha elimu ikiwa ni juhudi za kumuunga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

 

Akizungumza katika uzinduzi huo, balozi  huyo  amesema nchi yake itaendelea kusaidia Tanzania  katika shughuli za maendeleo hususani  kujenga ofisi  za walimu ili utoaji elimu bure kwa watoto wa Tanzania  uende sambamba na mazingira mazuri ya walimu.

 

Naye  Makonda amemshukuru balozi huyo akisema  China  imekuwa msatari wa mbele kwa kuiwezesha  Tanzania katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo na kuahidi kuendelea kuipa ushirikiano nchi hiyo kwa shughuli mbalimbali.

 

Aidha amewataka wananchi wa mkoa huo kuwapuuza viongozi wa kisiasa wanawaobeza wafadhili wanapotaka kujenga ofisi za walimu kwenye mkoa wake kwani waalimu ni watumishi wa umma na hawahusiani na masuala ya kisiasa.

 

NA DENIS MTIMA/GPL

 

 

 

Comments are closed.