The House of Favourite Newspapers

Balozi wa Tanzania Akanusha China Kudaiwa Kutaka Kufungua Vituo vya Polisi Nchini

0
Balozi wa Tanzania nchini China, Mberwa Kairuki.

 

BALOZI wa Tanzania nchini China, Mberwa Kairuki amekanusha taarifa zilizochapishwa na baadhi vya Vyombo vya Habari kwamba China inadaiwa kutaka kufungua Vituo vya Polisi nchini Tanzania “Taarifa hizi hazina ukweli wowote zipuuzwe”

 

Taarifa hiyo iliyochapishwa na Vyombo mbalimbali vya Habari ilisema China inadaiwa kufungua Vituo vya Polisi nchini Nigeria, Lesotho na Tanzania ili kudhibiti vitendo vya uhalifu vinavyofanywa na Raia wake wanaoishi katika nchi hizi tatu za Afrika.

 

Kwa upande wao Ubalozi wa China nchini Tanzania umekanusha pia taarifa hizo na kusema sio za kweli bali zimetungwa na baadhi ya Vyombo vya Habari vya Magharibi ili kuvuruga ushirikiano uliopo kati ya China na Afrika.

 

Ubalozi huo umesema China na Tanzania ni Marafiki wa muda mrefu kwenye maeneo yote na hawawezi kuyumbishwa na uzushi na kuvitaka Vyombo vya Habari vilivyosema vinautafuta Ubalozi kuthibitisha taarifa hiyo vifike Ubalozi “Mmesema mnataka kauli yetu, tupo hapa tunawasubiri”

ALI KAMWE AWASHUSHA VIWANGO SIMBA, AITOA DERBY KUWA MECHI NGUMU – ”LABDA NA AZAM”..

Leave A Reply