The House of Favourite Newspapers

Banana achukizwa na wasanii wanaopenda kiki

0

bananaStori: Uwazi Showbiz

MSANII mwenye uzito mkubwa kwenye Tasnia ya Muziki Bongo, Banana Zorro ‘Banana’ amefunguka kuwa miongoni mwa mambo anayochukizwa nayo kwenye tasnia ya muziki nchini ni kuwepo kwa lindi kubwa la wasanii wanaopenda kiki kuliko kufanya kazi.

Akichonga kiaina na gazeti hili Banana aliongeza kuwa kuwepo kwa wasanii hao kumesababisha pia Muziki wa Bongo Fleva kuzidi kupoteza hadhi yake ambayo ulikuwa umeanza kuipata na badala yake kuwa ni muziki ambao haudumu kwa muda mrefu. Msikie katika mahojiano yake kiaina aliyofanya na Uwazi Showbiz.

Uwazi Showbiz: Unadhani ni kwa nini wasanii wanapenda kiki kuliko kazi?

Banana: Nafikiri wengi wao wana maono ya hapa tu, hawaangalii mbele wanakokwenda.

Uwazi Showbiz: Unamaanisha nini?

Banana: Namaanisha wangekuwa wanaangalia wanakokwenda wasingeendekeza kiki kuliko kazi, wangekomaa kuboresha uwezo wao ambao ungewafanya kuendelea kukubalika hata bila kuwa na kiki. Wajifunze tu hata kutoka kwa wasanii ambao wamewatangulia, kwa mfano mimi, Mrisho Mpoto na wengine wengi ambao muda wote mashabiki wanataka kuzisikia kazi zao tu na si kiki zao.

Uwazi Showbiz: Unaweza kuwataja wasanii unaowafahamu wanaopenda kiki?

Banana: Ha! Ha! Haa! Acha kunichonganisha na watu, wao wenyewe wanajifahamu, haina hata haja ya kuwataja.

Uwazi Showbiz: Unawashauri nini?

Banana: Wafahamu muziki ni hazina ambayo mtu akiitumia vizuri anaweza kuishi kwa raha mustarehe milele ikiwa tu muziki wake utakuwa unaishi siku zote. Wakaze buti kunoa uwezo wao.

Leave A Reply