The House of Favourite Newspapers

BancABC Yashinda Tuzo ya Kuongoza Miamala Mitandaoni Tanzania

0

1c

Mkuu wa Kitengo cha wateja binafsi na wafanyabiashara wadogo wa BancABC, Bi. Joyce Malai akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar es salaam wakati wa kutoa taarifa rasmi kwa umma na wateja wa benki hiyo kuhusiana na ushindi wa tuzo waliyokabidhiwa na Visa hivi karibuni baada ya benki hiyo kuongoza katika miamala mitandaoni nchini Tanzania, hii inatokana na Visa kujiridhisha na ubora wa huduma ya benki hiyo hapa nchini. (Kulia) ni Mkuu wa kitengo cha Chaneli za huduma binafsi BancABC Silas Matoi.

2

Mkuu wa Kitengo cha wateja binafsi na wafanyabiashara wadogo wa BancABC, Bi.Joyce Malai akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar es salaam wakati wa kutoa taarifa rasmi kwa umma na wateja wa benki hiyo kuhusiana na ushindi wa tuzo waliyokabidhiwa na Visa hivi karibuni baada ya benki hiyo kuongoza katika miamala mitandaoni nchini Tanzania, hii inatokana na Visa kujiridhisha na ubora wa huduma ya benki hiyo hapa nchini. (Kushoto) ni Mkuu wa kitengo cha Masoko BancABC, Bi. Upendo Nkini na (kulia) ni Mkuu wa kitengo cha Chaneli za huduma binafsi BancABC Silas Matoi.

2b

Mkuu wa kitengo cha Chaneli za huduma binafsi BancABC, Silas Matoi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar es salaam wakati wa kutoa taarifa rasmi kwa umma na wateja wa benki hiyo kuhusiana na ushindi wa tuzo waliyokabidhiwa na Visa hivi karibuni baada ya benki hiyo kuongoza katika miamala mitandaoni nchini Tanzania, hii inatokana na Visa kujiridhisha na ubora wa huduma ya benki hiyo hapa nchini. (Katikati) ni Mkuu wa Kitengo cha wateja binafsi na wafanyabiashara wadogo wa BancABC, Bi.Joyce Malai na (wa kwanza kushoto) ni Mkuu wa kitengo cha Masoko BancABC, Bi. Upendo Nkini.

5

Mkuu wa kitengo cha Chaneli za huduma binafsi BancABC, Silas Matoi akifafanua kuhusu matumizi ya kadi ya ‘Visa Cash card’ inayomwezesha mteja kufanya malipo mitandaoni kwa urahisi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar es salaam wakati wa kutoa taarifa rasmi kwa umma kuhusiana na ushindi wa tuzo waliyokabidhiwa na Visa hivi karibuni baada ya benki hiyo kuongoza katika miamala mitandaoni nchini Tanzania, hii inatokana na Visa kujiridhisha na ubora wa huduma ya benki hiyo hapa nchini. (Katikati) ni Mkuu wa Kitengo cha wateja binafsi na wafanyabiashara wadogo wa BancABC, Bi. Joyce Malai na Mkuu wa kitengo cha Masoko BancABC, Upendo Nkini.

5b

Mkuu wa kitengo cha Chaneli za huduma binafsi BancABC Silas Matoi akifafanua kuhusu matumizi na faida za kadi ya ‘Visa Cash card’ inayomwezesha mteja kufanya malipo mitandaoni kwa urahisi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar es salaam wakati wa kutoa taarifa rasmi kwa umma na wateja wa benki hiyo kuhusiana na ushindi wa tuzo waliyokabidhiwa na Visa hivi karibuni baada ya benki hiyo kuongoza katika miamala mitandaoni nchini Tanzania, hii inatokana na Visa kujiridhisha na ubora wa huduma ya benki hiyo hapa nchini. (Katikati) ni Mkuu wa Kitengo cha wateja binafsi na wafanyabiashara wadogo wa BancABC, Bi. Joyce Malai. Jitihada za BancABC katika ubunifu, kuendeleza na kufanikisha usalama wa miamala matandaoni nchini Tanzania, imetambuliwa kwa tuzo ya Visa kuthibitisha ubora wa huduma yake mitandaoni.

6

(Toka kushoto) ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko BancABC Upendo Nkini, Mkuu wa Kitengo cha wateja binafsi na wafanyabiashara wadogo Bi.Joyce Malai na Mkuu wa kitengo cha Chaneli za huduma binafsi Silas Matoi wakionyesha tuzo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) waliyopewa na Visa hivi karibuni baada ya benki hiyo kuongoza katika miamala mitandaoni nchini Tanzania. Mkutano na waandishi wa habari umefanyika katika makao makuu ya benki hiyo mapema leo jijini Dar es salaam.

Mkuu wa Kitengo cha wateja binafsi na wafanyabiashara wadogo, Bi. Joyce Malai alithibitisha taarifa hiyo alipozungumza na vyombo vya habari mapema leo katika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es salaam.

“Tunafurahi kupokea tuzo hii licha ya ushindani wa masoko uliopo, hii inaonyesha ni jinsi gani tumejidhatiti kuhudumia wateja wetu na kuwarahisishia kufanya miamala ya kifedha,” alisema Bi. Malai.

Aliongeza kuwa katika jitihada hizi za kuboresha miamala salama mitandaoni, mtu yeyote anaweza kumiliki kadi hii ya Visa bila kujali kama anayo akaunti ya BancABC au la. Bi. Malai alifafanua kwamba kadi ya Visa ya BancABC ni rahisi kutumia kwani humhakikishia mteja ulinzi wa fedha zake na pia huondoa usumbufu wa kutembea na pesa taslimu.

Kadi hii inaweza kutumika kufanyia miamala mbalimbali ya kifedha kama vile kulipia tiketi za ndege pia kulipa posho na mishahara kwa wafanyakazi, kulipa ada za shule na kujikimu kwa wanafunzi, mikopo na misaada kwa serikali na mengineyo ili kupata kadi hii mteja anahitajika kuwa na kitambulisho halisi na kisha kujaza fomu zinazopatikana katika tawi lolote la benki hii.

Aliongeza kwamba wateja wanaweza kuweka fedha kwenye kadi hiyo kwa kutumia huduma mbalimbali za kutuma pesa kama vile TIGOPESA, AIRTELMONEY au M-PESA pamoja na benki zingine zilizopo Tanzania.

“Tunaamini kwamba upekee wa huduma hii ndicho kilichowavutia wateja na hivyo kusababisha ushindi wa tuzo ya Visa,” alisema.
Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Masoko BancABC, Bi. Upendo Nkini alisema, kadi hiyo inaweza kutumika pia kwa fedha za mataifa mbalimbali kama Shilingi ya Tanzania, Dola ya Kimarekani, Euro na Randi ya Afrika Kusini. “Licha ya kuwawezesha wateja kufanya biashara mitandaoni, Mteja anaweza kutumia pesa zake kwenye Visa ATM Zaidi ya 400 nchini au Visa ATM Zaidi ya 1.3 milioni duniani kote.

Zaidi ya hapo Visa inamawakala Zaidi ya 1000 Tanzania na mawakala Zaidi ya 35 milioni duniani kote. Kupata kadi hii tutumie barua pepe [email protected]
Atlas Mara iliinunua BancABC Juni 2014 huku ikizidi kujitanua Tanzania, Botswana, Mozambique, Zambia na Msumbiji. Baada ya hapo ilinunua benki mbili nchini Rwanda (BR Commercial na BPR ambazo zinaendelea kukamilisha mchakato wa kuungana).

KUHUSU KAMPUNI YA ABC
ABC Holdings Limited ni kampuni mama ya benki mbalimbali zilizopo kusini mwa Jangwa la Sahara zinazofanya kazi chini ya Benki ya ABC na kutoa huduma za kipesa ikiwamo kuhudumia watu binafsi, biashara na mashirika ya kibenki, vilevile umiliki wa mali usitishaji wa hisa na huduma za hazina.
Mwaka 2014, Atlas Mara ilipata wadau wengi katika ABC Holdings, ikiongozwa na wataalamu wake, watu, ugunduzi, shauku na uadilifu katika huduma zake. ABC inatimiza ndoto zake za kuwa mshirika makini Afrika kwa kutoa huduma bora duniani zitakazowafaidisha wadau wake wote.
www.bancabc.com

KUHUSU ATLAS MARA
Atlas Mara iliorodheshwa katika Soko la Hisa London, mwezi Desemba 2013. Ndoto za kampuni hii ni kuanzisha taasisi kubwa ya kifedha Kusini mwa Sahara kupitia uzoefu wake, umahiri na upatikanaji wa mitaji, ukwasi na uzalishaji fedha. Malengo yakiwa ni kujumuisha ujuzi wa taasisi za dunia nzima na mitazamo ya kina ndani ya Afrika, hivyo kusaidia kukuza uchumi katika nchi zinazo hudumiwa na Kampuni hii.
www.atlasmara.com

Leave A Reply