The House of Favourite Newspapers

Katibu Wizara ya Afya ‘Awawakia’ Waganga wa Tiba Asilia

0

1.Katibu Mkuu Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Michael O.John akisoma taarifa yake kwa wanahabari (hawapo pichani).Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Michael O. John akisoma taarifa yake mbele ya wanahabari (hawapo pichani).

IKIWA Agosti 31, ya kila mwaka ni siku ya kuadhimisha kilele cha siku ya Tiba ya Asili ya Mwafirika, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Michael O. John amewashauri waganga wa tiba za asili kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zinazowasimamia katika kuhakikisha bidhaa zitumiwazo zinakuwa zimesajiliwa huku akiwaagiza kuondoa mabango yao ya biashara yaliyokaa kiholela.

Hayo ameyasema katibu huyo leo alipokuwa akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam ambapo alisema maadhimisho ya siku ya Tiba ya Mwafrika yalianza rasmi mwaka 2003 baada ya Mawaziri wa Afya wa Nchi Wanachama wa Shirika la Afya Duniani Kanda ya Afrika kuridhia kuwepo kwa sherehe hizo kwa zaidi ya nchi 46 kutoka Kanda ya Afrika.

2.Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Aidha amesema Tanzania inaadhimisha siku hii kwa mambo makuu manne ambayo ni kujenga na kufufua heshima ya huduma za tiba asili ambazo historia inaonesha zinakandamizwa na kudharaulika.

Pili serikali kuhamasisha waganga wa tiba asili kujiepusha migongano katika jamii kwa kukutohusisha ushirikina na uchawi kama chanzo cha ugonjwa pamoja na mengine aliyoyataja.

Kauli mbiu katika maadhimisho hayo ni ‘Kanuni za Udhibiti wa Bidhaa za Tiba Asili Katika Kanda ya Afrika’ ambayo inalenga kusimamia katika suala zima la kuratibu kanuni na taratibu kusajili kudhibiti bidhaa zitumiwazo katika huduma za tiba asili nchini.

Vilevile amewaasa waganga wa tiba asili kuzingatia sera, sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa kuachana na matangazo yasiyofaa, kuacha kuweka mabango hovyo barabarani huku akisema matangazo ya redioni ni lazima yapate kibali kutoka Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala.

NA DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply