The House of Favourite Newspapers

Banda Avutiwa na Utengenezaji wa Magazeti Ya Global (Picha)

Beki Mtanzania, Abdi Banda, anayecheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini katika Klabu ya Baroka  akiangalia picha kwa Msanifu kurasa, Shaffih Hashim.

BEKI Mtanzania, Abdi Banda, anayecheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini katika Klabu ya Baroka, alivutiwa na matayarisho na utengenezaji wa magazeti wa Global Publishers alipotembelea ofisi za Global Group zilizopo Sinza Mori jijini Dar hivi karibuni.

…Banda akiendelea kutazama.

Akiongea na mtandao wa Global Publishers, mchezaji huyo alisema “nimevutiwa na  jinsi wasanifu kurasa wa Global Publishers  wanavyofanya kazi kwa ubunifu mkubwa kulinganisha na ambao nilishawaona katika media mbalimbali nilizowahi kuzitembelea.”

Aliwashauri Watanzania wanunue magazeti ya Global Publishers ambayo ni Amani, Risasi Mchanganyiko, Uwazi, Ijumaa Wikienda,  Championi na Spoti Xtra ili kujionea uhondo uliomo.

….Akifuatilia kinachoendelea.
…Akiagana na Shaffih Hashim.
…Akiwa kwa msanifu kurasa, Ayoub Dotto.
…Akifuatilia kazi za msanifu Glory Masawe.

 (PICHA: SWEETBERT LUKONGE | GLOBAL PUBLISHERS)

Comments are closed.