The House of Favourite Newspapers

Banka Rasmi Uwanjani Yanga Leo, Zahera Ampa Majukumu

Mohammed Issa ‘Banka’

KIUNGO mchezeshaji mpya wa Yanga, Mohammed Issa ‘Banka’, rasmi anatarajiwa kuonekana uwanjani leo Jumapili hii katika mchezo wa Ligi Kuu Bara baada ya kumaliza adhabu yake ya kifungo.

 

Banka alifungiwa na Kamati ya Kuzuia na Kupambana na Dawa Zisizoruhusiwa Michezoni ya Kanda ya Tano Afrika (RADO) ambayo ilitoa hukumu ya kum­fungia mwaka mmoja baada ya kugundulika kwenye michuano ya Cecafa.

 

Kiungo huyo aliyesajiliwa na Yanga kwenye msimu huu wa ligi akitokea Mtibwa Sugar, leo Al­hamisi rasmi adhabu inamalizika huku akitarajiwa kuanza kuvalia jezi ya kijani na njano katika mch­ezo ujao wa ligi timu hiyo itaka­pocheza dhidi ya JKT Tanzania, Mkwakwani, Tanga.

 

Akizungumza na Championi Iju­maa, Mratibu wa Simba, Hafidh Saleh, alisema kiungo huyo rasmi ataonekana uwanjani katika mchezo unaofuatia wa ligi dhidi ya JKT Tanzania utakaopigwa Jumapili hii kwenye Uwanja wa Mkwakwani.

 

Saleh alisema kiungo huyo muda mrefu alikuwa tayari ameingiziwa mfumo na programu za Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera katika mazoezi yake ya kila siku aliyokuwa ana­wafanyisha wachezaji wake.

 

“Adhabu ya Banka ime­malizika katika kipin­di kizuri ambacho timu inamhitaji, kama unavyoona ratiba ilivyotubana ya ligi, wachezaji tunacheza mechi hiyo keshokut­wa tunacheza nyingine huku tukisafiri mwendo mrefu,” al­isema Saleh.

Comments are closed.