The House of Favourite Newspapers

Barabara ya Juu (Fly Over) Kujengwa Tazara, Dar

0

 Ramani ya Barabara ya Juu (Fly Over) itakavyokuwa baada ya ujenzi kukamilika unaoanza mwezi ujao kukamilika Oktoba  2018. Mkataba wa ujenzi wa barabara hiyo utakaogharimu sh. bilioni 100 umesainiwa jana chini ya usimamizi wa Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli

 Waziri wa Ujenzi, ambaye pia ni Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli (aliyesimama katikati) akishuhudia utiaji wa saini mkataba wa ujenzi wa barabara ya juu (Fly Over) katika makutano ya barabara za Mandela na Nyerere Tazara, Dar es Salaam jana. Wanaotia saini ni Meneja Mkuu wa Kampuni ya Sumitomo Mitsui itakayojenga barabara hiyo, Ichiro Aoki (kushoto) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara wa Serikali, Patrick  Mfugale. Ujenzi huo unaotarajia kuanza hivi karibuni  na kugharimu zaidi ya Bilioni 100 utakamilika Oktoba  2018.

Muonekano wa barabara hiyo.Fly Over ya Tazara itakavyokuwa.Magufuli akialimiana na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Sumitomo Mitsui itakayojenga barabara hiyo, Ichiro Aoki.Dk Magufuli akizungumza wataki wa utiaji saini mkataba huo

 (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA)

Leave A Reply