The House of Favourite Newspapers

Barabara za kuingia Stendi za Simu 2000, Makumbusho zalalamikiwa

0

BARABARA za kuingia stendi za mabasi ya daladala Simu 2000 na Makumbusho jijini Dar es Salaam zinalalamikiwa kwa kuwa na mashimo makubwa yanayohatarisha usalama.

Baadhi ya wananchi wakiwemo madereva wa daladala waliozungumza na waandishi wetu walisema barabara hizo ni hatarishi kwa sababu zinaweza kusababisha ajali.

“Barabara ya kuingia Stendi 2000 ina mashimo makubwa. Kuna shimo moja ambalo madereva huwa tunalikwepa na kusababisha adha kubwa, linaweza kusababisha ajali,” alisema dereva mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Mohamed Ali ayanefanya safari zake kutoka kituoni hapo hadi Tegeta.

Naye dereva mwingine aliyejitambulisha kwa jina moja la Charles alisema anashangaa kuona serikali haiijali barabara hiyo wakati inaingiza fedha kwani mabasi yote yanayoingia humo hulipiwa.

Naye dereva mwingine Yahya Khamisi anayefanya safari zake kutoka Makumbusho kwenda  Buguruni alisema barabara za kuingia kituo hicho ni mbovu na hata kituo chenyewe inaponyesha mvua hujaa tope.

“Haya ni mambo ambayo yanahitaji kufanyiwa kazi na siyo lazima aseme Rais John Magufuli. Kwani viongozi hawaoni? Tunalipa kila siku kuingia kituoni, fedha zinafanya kazi gani?” alihoji.

Mkandarasi Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Baraka Mkuya, akizungumzia tatizo hilo aliwahi kusema kazi ya kuweka lami katika barabara ya kuingilia katika Kituo cha Simu 2000 ipo katika bajeti ya fedha ya mwaka huu.

KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP

*********

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

ERIC SHIGONGO INSTAGRAM: @ericshigongo

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: Global TV Online

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE:@shigongotz

Leave A Reply