The House of Favourite Newspapers

Barabara Jijini Dar Zapungua Foleni

dar-1

Hali ilivyoonekana mchana wa leo Barabara ya Bibi Titi jijini Dar.

dar-2

Barabara ya kuelekea Posta Mpya nayo ilivyoonekana kutokuwa na foleni.

dar-3

Taswira mbalimbali za barabara za Posta zilivyoonekana mchana wa leo ambapo misururu ya magari ilikuwa karibu haipo.

dar-4

Watembea kwa miguu wakionekana kuvuka barabara inayotokea maeneo ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iitwayo  Bibi Titi kwenye mataa ya Barabara ya  Morogoro karibu na maduka ya City Mall.

dar-5

Barabara ya Morogoro eneo la Chuo cha Dar es S Salaam Institute Of Technology (DIT) ilivyoonekana kutokuwa na msongamano wa magari.

dar-6

Na Denis Mtima/GPL

MTANDAO huu ulipopita katika barabara mbalimbali jijini Dar es Salaam leo, umebaini kwamba zile foleni ambazo kila mara na kila siku huwa kero kubwa kwa wakazi wa jiji hili kwa kuwachelewesha katika shughuli zao mbalimbali, hivi sasa zimeonekana waziwazi kupungua.

Uchunguzi uliofanywa kwa kuhoji watu mbalimbali kuhusu kupungua kwa foleni hizo, umeonyesha kwamba hivi sasa watu wengi, hususan wafanyakazi katika sekta za serikali na binafsi wako katika mapumziko ya Krismasi na Mwaka Mpya, wengi wao wakiwa hapahapa jijini na wengine wakiwa wamekwenda mikoani kwa ajili ya mapumziko hayo na kusalimia ndugu na jamaa.

Comments are closed.