The House of Favourite Newspapers

Baraza aipa sare Dabi ya Kariakoo

0

Aliyekuwa Kocha mkuu wa Biashara United, Kagera Sugar zote za hapa Tanzania Francis Baraza amesema kuelekea mchezo wa dabi ya kariakoo baina ya Simba na Yanga anaamini mchezo huo utamalizika kwa sare kutokana na timu hizo mbili kucheza kwa kiwango cha juu katika michezo yao waliyoicheza hivi karibuni.

Akizungumza na GlobalPublishers Baraza ambaye kwa sasa ni Kocha wa timu ya Polisi FC ya Kenya ameema “Mchezo wa dabi ya Simba na Yanga ni mchezo mgumu ambao hufuatilia kwa ukaribu Zaidi na wananchi wa mataifa ya ukanda huu wa afrika mashariki na kati hivyo ninachoweza kucheza ni kwamba mchezo huo utamalizika kwa sare kutokana na viwango ambavyo vimeonyeshwa na timu hizo kwa michezo ya karibuni”

“Simba mchezo wao wa mwisho waliwafunga Ihefu bao 2-0 kule Mbeya na Yanga waliifunga Kagera Sugar bao 5-0 hivyo kwa mwenendo huu inathibitisha kwamba mchezo wa jumapili utakua na ugumu kwa kiasi gani kwakua timu zote ziko juu kuelekea mchezo utakaozikutanisha timu hizo”

“lakini kiufundi mchezo huu utaamuliwa na makocha wenyewe kwakua ukiangalia Simba baada ya kumpata kocha Robertinho imebadilika sana na Yanga chini ya kocha Nesredine Nabi imekuwa na kiwango bora hivyo pamoja na vita ya wachezaji kwa wachezaji pia kutakua na vita kubwa ya kiufundi baina ya makocha hawa wawili lakini naamini kwamba mchezo ule utamalizika kwa timu kutoka sare”

 

Leave A Reply