The House of Favourite Newspapers

Barnaba Adai Ruge Mutahaba Alimlea, Asimulia Safari Yake ya Muziki Hadi Hapo Alipofikia

0
Marehemu Ruge Mutahaba

MSANII wa Bongo Fleva, Barnaba Classic amesema mtu aliyemlea katika Sanaa ya muziki na kumfanya kuwa staa ni aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media, marehemu Ruge Mutahaba.

 

Barnaba amesema hayo usiku wa kumkia leo, wakati wa hafla ya kuitambulisha Album yake mpya ya Love Sound Different ambapo watu mbalimbali wakiwemo wasanii na viongozi wa siasa walihudhuria.

Barnaba Classic

“Baada ya kutoka nyumbani kwa Baba na Mama na kuingia kwenye industry ya muziki nilipokelewa na kulelewa na Ruge Mutahaba ambaye kwa sasa ni marehemu na yuko mbele za haki, tunafahamu hayuko nasi lakini leo tuko naye hapa kinafsi na kiroho.

 

“Safari yangu ya muziki kutoka nyumbani kwenda mtaani, kila mtu alikuwa anajua Barnaba anafahamu muziki, lakini kama ninavyosema, watu wanaleta vitu, “you can’t be someone without somewhere’ lazima upate watu ndipo upate kitu.

 

“Nilipenda muziki nikiwa mtaani, kitu nilichokipenda sio kuimba vizuri tu lakini ni mahusiano mazuri na watu. Hata leo kuna sura unaziona hapa unashangaa huyu naye amekuja kwenye shughuli ya Barnaba?” amesema Barnaba.

Leave A Reply