The House of Favourite Newspapers

Barnaba afungukia mkumbo wa kushuti Sauz

0

barnaba1Stori: Uwazi Showbiz

MKALI katika gemu la Muziki wa Bongo Fleva, Elius Barnabas ‘Barnaba’ hivi karibuni amefungukia uamuzi wake wa kwenda kushuti video yake mpya ya wimbo uitwao Lover Boy nchini Sauz kuwa umesababishwa na ushindani uliopo kwenye muziki kwa sasa wa wasanii kuchuana kwa vichupa vikali.

Akistorisha kupitia gazeti hili, Barnaba anayemiliki studio iitwayo High Table Sound alisema kuwa hata kwa msanii asiyependa kushuti Sauz analazimika kufuata mkumbo huo ili kuchuana na wasanii wengine wanaopiga hatua kwa sababu tu wameshuti video zao pande hizo.

“Wimbo wangu mpya nimeshutia Sauz, nimelazimika kufuata mkumbo ili na mimi nizidi kupiga hatua katika kazi zangu ikiwa ni pamoja na kutengeneza koneksheni na madairekta wapya kutoka nje,” alimaliza Barnaba bila kumuweka wazi dairekta aliyeshuti kichupa hicho maana bado hakijatoka.

Leave A Reply