The House of Favourite Newspapers

BARNABA ALIA WIVU LIVE KWA MKEWE

0

wivu ni kidondaWahenga walinena wivu ni kidonda, ukishiriki utakonda. Hivi ndivyo unavyoweza kusema ukikutana na kibao kipya kutoka kwa Barnaba Classic katika kibao chake kipya kinachokwenda kwa jina la Mapenzi Jeneza, ambacho ndani yake kumejaa mistari yenye kuonyesha wivu laivu na bila kusahau stress, hasa baada ya kumwagana na mke wake, Zuu Namela.

“Yatakwisha hizo nyodo za kupostiana Instagram, mara Snapchat, mara Facebook, najikuta nashindwa kuna muda nawaza upumbavu.
“Vile ulivyonibidua naye unambidua vilevile, sasa nawaza vile ulivyonihemea naye unamhemea vilevile, ni mawazo tu sina plan za kurudi, mapenzi yanauma, na moyo siyo chuma, na mapenzi hayana komando na moyo wangu kaubeba kwenye Rambo.

wivu ni kidonda
Aliyekuwa mke wa Barnaba Zuu Namela, akiwa na mpenzi wake wa sasa Brown

“Yatakwisha hizo nyodo, napiga simu unajitia hunijui, mara unakata, mara unampa mpenzi wako kunitukana”
Hiyo ni baadhi ya mistari inayopatikana kwenye ngoma hiyo ya Mapenzi Jeneza, ambayo imewafanya mashabiki wagundue kwamba Barnaba bado ana mawazo na wivu juu ya mkewe, ambaye kwa sasa ni mpenzi wa mwanamuziki chipukizi anayeitwa Brown.

NA ISRI MOHAMED/GPL

Leave A Reply