The House of Favourite Newspapers

Bashe Atoa Kauli Nzito Sakata La Sukari – ”Wafanyabiashara 28 Tumewakamata -Tumeshawabeba Sana” – Video

0
Waziri wa Kilimo, Hussein Mohamed Bashe akizungumza na Wahariri pamoja na Waandishi wa Vyombo mbalimbali waliohudhuria mkutano ulioandaliwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 22 Februari, 2024

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema licha ya tatizo la uhaba nchini lililosababishwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kunyesha kwa mvua nyingi, bado kuna changamoto ya baadhi ya wafanyabiashara ambao wanafanya uhuni kwa kuuza bei tofauti na iliyoelekezwa na serikali.

Bashe amesema wamebaini kwamba, waingizaji wa sukari nchini, huwauzia wafanyabiashara wa kati sukari kwa bei elekezi lakini wao huenda kuuza kwa bei ghali kwa walaji wa mwisho na kusababisha kero kwa wananchi.

Amesema mpaka sasa wameshawakamata wafanyabiashara 84 ambao watafikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayowakabili na zoezi la kuwatafuta wengine wanaohujumu mpango wa serikali kushusha bei ya sukari linaendelea.

Leave A Reply