The House of Favourite Newspapers

Breaking News: Basi la Luwinzo lapata ajali Mufindi

2

luwinzo (1) luwinzo (2)Ajali ilivyotokea mapema leo asubuhi.
luwinzo (4)Shughuli za kuwaokoa walionusurika na ajali.

AJALI mbaya imetokea leo asubuhi baada ya basi la abiria mali ya Kampuni ya Luwinzo linalofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Njombe, kugongana na lori wakati basi hilo likiwa linatoka Njombe kuelekea Dar es Salaam na kusababisha watu kadhaa kupoteza maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Ajali imetokea katika eneo la Kinegembasi, Kata ya Mbalamaziwa wilayani Mufindi mkoani Njombe.

2 Comments
  1. Moses says

    dah nyie madereva wa mabasi jitahidin kuwa makini tafadhalin sana

  2. Msomi says

    Hizi ajali za magari barabarani zimeua wananchi wetu wengi sana kwa muda mrefu sana. Mara zote tumezoea kusikia viongozi wakitoa rambirambi tu kwa Wakuu wa mikoa na familia. Hii haitoshi. Tunaomba Rais wetu, au Waziri Mkuu, alivalie njuga suala hili ili kutafuta njia za kupunguza vifo vya aina hii. Ni jipu kubwa hili na lazima litumbuliwe. Sasa tuseme imetosha wananchi kufa hovyohovyo namna hii kila kukicha!

Leave A Reply