The House of Favourite Newspapers

Bifu la Iggy Azalea na Bhabie Lafikia Pabaya, Tazama Alichofanyiwa (VIDEO)

Rapaz wawili wa kike Iggy Azalea na Danielle Bregoli maarufu kama Bhad Bhabie limefikia pabaya baada ya Bhabie kumshambulia mwenzake kwa kumwagia maji wakiwa kwenye uzinduzi wa shoo ya mavazi ya Cardi B huko Los Angeles usiku wa Novemba 14, mwaka huu.

 

Kipande cha video kilichowekwa mtandaoni kinamwonyesha Bhabie akirusha kikombe cha maji kuelekea kwa rapa mwenzake Iggy Azalea

 

Alichokisema Bhabie baada ya kufanya kitendo hichi ni, “Alikuwa anaongea upumbavu kwenye Instagram, simhofii huyo kahaba, nimefanya lile nalotakiwa kulifanya.

 

Kwa upande wa Iggy alifunguka na kusema, “Nadhani ilikuwa sio pombe. Bado hajakuwa, ni mtoto.

 

Bifu la wawili hao lilianza Septemba mwaka huu baada ya Iggy Azalea ku-share post yenye tarehe za Tour yake lakini Bhabie alimkebehi kwenye mtandao huo huo wa Instagram.

NABII Shillah Afunguka Mazito/Ataja Watu Waajabu Wanamfuatilia

Comments are closed.