The House of Favourite Newspapers

Bei Za Kupiga Picha Daraja La Nyerere, Kigamboni

0
Muonekano wa daraja la Nyerere Kigamboni.

Baada ya kuwepo kwa mkanganyiko wa gharama za kupiga picha kwenye daraja la Nyerere Kigamboni hatimaye serikali imetangaza mchanganuo wa malipo ya huduma hiyo darajani hapo.

 

Kaimu meneja mahusiano wa NSSF Salim Khalfan Kimaro, amesema Serikali imetoa utaratibu huo maalumu ambao watu wanaotaka huduma ya picha katika daraja hilo watautumia, ambapo pia amesema uamzi huo umezingatia suala zima la kulinda miundombinu ya daraja hilo pamoja na usalama wa raia wenyewe..

 

Utaratibu wa sasa wapiga picha watalazimika kuomba kibali kwenye Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, kisha watapata maelekezo ya kufuata.

Aidha gharama za upigaji picha kwa matukio maalum kama harusi, kutengeneza video za kwaya na wasanii wa mziki wa kawaida itakuwa ni Tsh 250,000 kwa saa moja na Tsh 125,000 kwa nusu saa.

 

Kwa upande wa wapiga picha za kawiada kwa mtu mmoja mmoja (selfie) hawatalipia gharama yoyote, lakini wametahadharishwa kuwa makini na usalama wao ili kuepuka athari zinazoweza kujitokeza.

Leave A Reply