The House of Favourite Newspapers

Beki Atangaza Vita ya Namba Yanga SC

BEKI wa kushoto wa Yanga, Gadiel Michael, ametangaza vita kufuatia kauli yake kwamba atajituma kuhakikisha anamshawishi kocha kumpa namba ya kudumu katika kikosi cha timu hiyo.

Michael ambaye ametokea Azam FC tangu atue katika kikosi hicho ameonekana kuaminiwa na kocha George Lwandamina ambapo kume­sababisha kumweka benchi Haji Mwinyi.

 

Akizungumza na Champio­ni Jumatano, Gadiel alisema kwa sasa anachoangalia katika timu yake hiyo ni kuhakikisha anaji­tuma kwa nguvu zote ili aweze kuendelea kujihakikishia nafasi.

“Tunashukuru Mungu kuweza kufanikiwa kuibuka na ushindi dhidi ya St Louis na tume­fanya vile ambavyo kocha alituelekeza na ninaamini tutafanya vyema katika mchezo unaofuata.

 

“Bado sijajiimarisha zaidi katika nafasi yangu hii la­kini nahitaji kujituma zaidi ili niweze kuwa bora zaidi na zaidi na iwapo mwenye namba atarejea (kwenye kiwan­go), mwalimu ndiye aamue am­pange nani lakini hakika nataka kujituma sana kila mmoja aone kazi yangu.

“Kujituma ndiyo siri ya mafanikio, naamini nitakuwa bora kwa kuhakikisha na­fanya kile mwalimu anach­okitaka,” alisema Gadiel.

 

 Khadija Mngwai, Dar es Salaam

VIDEO: KAMATI YA NIDHAMU YAMSHINDILIA NYOSSO

Comments are closed.