Beki Mbrazil wa Simba Kazi Wanayo!

SIMBA jana mchana waliposti posti ya usajili wao mpya kwenye mtandao wao, Yanga wakaanza kusonya na kubeza wakidhani ni straika Msauzi aliyefulia, Ryan Moon, kumbe wanafanana kwa mbaali.

 

Waliyemshusha Simba ni beki Mbrazil, Gerson Fraga Vieira ambaye kwa mujibu wa mtandao wa thamani ya wachezaji, bei yake ni Sh.700mil na faili lake linaonyesha ni jembe kwelikweli.

 

Mchezaji huyo amemaliza mkataba wake na klabu ya ATK inayocheza Ligi Kuu India, ambapo ni beki mahiri wa kati. Gerson aliyezaliwa Brazil mwaka 1992, alichezea klabu mbalimbali za nchini humo, India, Uruguay na Ufaransa.

 

Mwaka 2013, alichezea Red Bull ya Brazil, 2014 akajiunga na Atenas ya Uruguay kwa mkopo. Msimu wa 2016 aliibukia kwenye Ligi Kuu ya India katika klabu ya Mumbai City, mwaka unaofuata akarudi Brazil kujiunga na Atletico Tubarao kabla ya kurejea tena Mumbai City msimu wa 2017/18.

 

Baadae akasitisha mkataba na timu hiyo na kwenye Ligi Daraja la Pili Japan alikojiunga na Renofa Yamaguchi, mwaka jana. Julai 2018.

 

Gerson alirudia tena India na kujiunga na ATK ambayo alikuwa nayo mpaka Simba wanamnasa. Rekodi zake zinaonyesha kwamba kwenye timu za vijana za Brazil za U-15 na U-17 amewahi kucheza na mastaa wakubwa akiwemo Neymar.

 

Simba wanatarajia kumalizana na mchezaji huyo muda wowote kwani jana walidokeza kwamba alikuwa angani kuja Dar es Salaam kusaini.

 

Mawakala wa kimataifa wamewaambia Simba kwamba mchezaji huyo licha ya kwamba watamlipa hela kubwa lakini ni mchezaji makini kwenye safu ya ulinzi na anayewafaa kwa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwani ana uzoefu wa mechi kubwa na anajua kufunga.

TFF Yashindwa ‘KUJIZUIA’ Yawajibu Wanaomsema Kocha AMUNIKE “Mnawakatisha Tamaa”

Loading...

Toa comment