The House of Favourite Newspapers

Benchi La Ufundi Simba Kikaangoni Bodi ya Wakurugenzi Kukutana

0
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Salim Muhene ‘Try Again’.

BODI ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba, imepanga kukutana kwa ajili ya kulifanyia tathimini Benchi la Ufundi la timu hiyo, linaloongozwa na Kocha Mkuu, Mbrazili, Roberto Oliveira ‘Robertinho’.

Hiyo ni baada ya Simba kutoka kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Azam katika mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports uliopigwa juzi Jumapili kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.

Kupoteza mchezo huo, ni wazi msimu huu Simba inaumaliza bila ya kombe lolote kutokana na kuyawania mataji matano ambayo ni Ngao ya Jamii, Ligi Kuu Bara, Kombe la Shirikisho la Azam Sports, Kombe la Mapinduzi na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akizungumza na Spoti Xtra, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, alisema mara baada ya mchezo dhidi ya Azam FC, haraka uongozi utakutana kufanya tathimini ya kila kiongozi wa Benchi la Ufundi.

Ally alisema upo uwezekano mkubwa wa kuingiza maingizo mapya ya viongozi wa benchi la ufundi katika msimu ujao wenye maono na kuifikisha pazuri katika michuano ya kimataifa.

Aliongeza kuwa, baada ya tathimini hiyo kufanywa ya viongozi, haraka watakuja na majibu mazuri kwa mashabiki wao kuelekea msimu ujao ambao ni lazima wabebe makombe yote ya ndani.

“Tumeumizwa na matokeo haya mabaya ya kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Azam FC, kwa kifupi tumeumaliza mwendo msimu huu tukiwa tumekosa makombe yote na badala yake tujipange kwa ajili ya msimu ujao.

“Baada ya kuondolewa, haraka uongozi umepanga kukutana kwa ajili ya kulifanyia tathimini benchi la ufundi, kwani ni lazima tuwe na viongozi wa ufundi wenye malengo ya kufika hatua ya Nusu Fainali ya michuano ya kimataifa na sio Robo Faiinali pekee.

“Hivyo mara baada ya kukuatana uongozi kufanya tathimini hiyo, haraka tutakuja na majibu ya nini kimeamuliwa kwa ajili ya kuijenga upya timu,” alisema Ally.

STORI: WILBERT MOLANDI

”HAKUNA HASARA KWENYE MANUNUZI SGR TABORA – KIGOMA, HATUWEZI KUVUNJA MKATABA” – NAIBU WAZIRI…

Leave A Reply