The House of Favourite Newspapers

Benchikha Abadili Maamuzi, Ambakisha Luis

0

DAKIKA 45 zimetosha kumshawishi Kocha Mkuu wa Simba, Mualgeria, Abdelhak Benchikha kumbakisha kiungo wake mshambuliaji, Luis Miqquissone katika timu hiyo.

Luis alikuwepo katika orodha ya wachezaji wa timu hiyo, watakaochwa katika dirisha hili dogo lililofunguliwa Desemba 12, mwaka jana.

Nyota huyo juzi akitokea benchi, alionyesha kiwango bora walipovaana dhidi ya Singida Fountain Gate waliowafunga mabao 2-0 huku Luis akifunga moja kati hayo kwa shuti kali nje ya 18.

Taarifa ambazo imezipata Championi Jumamosi, Benchikha amefuraishwa na mabadiliko ya kiwango cha kiungo huyo katika mchezo dhidi ya Singida Fountain Gate huku akimpa nafasi kuongeza ubora wake katika michezo ijayo.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa baada ya mchezo huo dhidi ya Singida Fountain Gate, kocha huyo alifanya kikao na nyota akimtaka kuongeza bidii ya mazoezi zaidi na kucheza kwa kufauata maelekezo yake.

Aliongeza kuwa kiungo huyo amepewa muda huo kuongeza kiwango chake zaidi baada ya kukaa muda mrefu bila kucheza, akimtaka kutumia Kombe la Mapinduzi kurejesha ubora wake.

“Mipango ya Luis kuachwa katika dirisha hili dogo imeondolewa na haitakuwepo tena, baada ya kufurahishwa na mabadiliko ya kiwango chake.

“Baada ya mchezo dhidi ya Singida Fountain Gate, kocha alizungumza na Luis mambo kadhaa kati ya hayo kumtaka kutumia Kombe la Mapinduzi kurejesha kiwango chake ambacho alikuwa nacho awali.

“Kocha anaamini uwezo wa Luis, lakini kukaa nje ya uwanja kabla ya kusajiliwa Simba ndiyo kumeshusha kiwango chake, hivyo ni muda kwake kurejesha mechi fitinesi yake Mapinduzi,” alisema mtoa taarifa huyo.

Akizungumzia hilo Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alisema kuwa: “Luis yupo na ataendelea kuwepo Simba, hizo taarifa zilizokuwa zinaendelea ni tetesi, juzi alifunga bao zuri dhidi ya Singida Fountain Gate, ambalo ninaamini huenda likawa bao bora la mashindano.”

STORI NA WILBERT MOLANDI

RAIS SAMIA AMTUMBUA BOSI wa WIZARA ya NISHATI – SONGORA – ATAPANGIWA KAZI NYINGINE…

Leave A Reply