The House of Favourite Newspapers

Benki ya ACB Yahudhuria Mkutano wa Wadau Wake wa Rombo Waishio Dar

0
Meneja Masoko wa ACB Makao Makuu, Innocent Ishengoma akizungumza kwenye mkutano huo.

Kikundi cha kusaidiana cha wenyeji wa Rombo mkoani Kilimanjaro kiitwacho Keni Upendo Family wamefanya mkutano wa mwaka kujadili mambo mbalimbali ya maendeleo ya kikundi hicho.

Katika mkutano huo kikundi hicho kimeihusisha benki ya Akiba Commercial (ACB) ambayo ndiyo wanayohifadhia fedha zao ambapo benki hiyo iliwakilishwa na Meneja Masoko wake, Innocent Ishengoma kutoka Makao Makuu.

Mmoja wa viongozi wa kikundi hicho akimuuliza maswali Ishengoma.

Wanakikundi hao walimuuliza Ishengoma maswali mbalimbali ya usalama wa fedha zao na kuishauri benki hiyo kuboresha huduma zake ingawa walikiri ubora wanaoupata kwenye benki hiyo.

Ishengoma akijibu maswali ya wanakikundi hao aliwatangazia huduma yao mpya ya kulipia malipo ya serikali kupitia benki hiyo.

Ishengoma akikabiliana na maswali ya wajumbe.

Ishengoma alisema malipo hayo ni pamoja na faini za polisi, malipo ya Mamlaka ya Mapato (TRA) kulipia bili za maji, umeme na malipo mengine. Alisema Ishengoma.

Ishengoma akijibu maswali ya wanakikundi hao na kuwaelezo maboresho makubwa yaliyofanyika kwenye benki hiyo.

Pamoja na huduma hiyo Ishengoma amewaambia wadau hao kuwa wako katika hatua za mwisho kukamilisha huduma yao ya kuwaweka mawakala nchini nzima ili kuwafikia wateja wao kiurahisi. Alimaliza kusema.

Baadhi ya viongozi wa kikundi hicho wakimsikiliza kiumakini Ishengoma (hayupo pichani) alipokuwa akitoa ufafanuzi juu ya uboreshwaji wa huduma zao.                                            HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS /GPL 
Leave A Reply