Benki ya Biashara ya DCB yang’ara tuzo za NBAA
Benki ya Biashara ya DCB imeahidi kuendelea kubuni na kuboresha huduma na bidhaa zake hususani huduma za kidigitaji ili iendelee kungara katika tuzo zijazo za Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Mahesabu (NBAA).
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Biashara wa benki hiyo, James Ngaluko, mara baada ya benki hiyo kukabidhiwa tuzo za NBAA katika kipengele cha mabenki madogo na ya ukubwa wa kati, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi.
Naye akizugumza katika hafla ya kupokea tuzo hizo, Mkurugenzi wa Fedha wa benki hiyo, Zacharia Kapama alisema wamekuwa wakishinda tuzo hizo kwa miaka mitatu mfululizo na hiyo imetokana na kuzingatia viwango vya kitaifa na kimataifa katika utoaji wa taarifa za usimamizi wa fedha.
Comments are closed.