The House of Favourite Newspapers

BENKI YA CBA YAZINDUA TAWI JIPYA SAYANSI KIJITONYAMA

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya CBA, Gift Shoko na Mteja wa benki hiyo Justina Mashiba wakikata utepe kuzindua tawi jipya la beni hiyo lililopo Sayansi Kijitonyama Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa kitengo cha Wateja Binafsi Julius Konyani.
Mteja wa Bneki ya CBA kutoka Kampuni ya Universal Communication, Justina Mashiba akizungumza kwa niaba ya wateja wengine wakati wa hafla ya kuzindua tawi jipya la benki hiyo lililopo Sayansi Kijitonyama Dar es Salaam.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya CBA, Gift Shoko akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua tawi jipya la benki hiyo lililopo Sayansi Kijitonyama Dar es Salaam.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya CBA, Gift Shoko (kulia) akizungumza na mteja wa benki hiyo, Justina Mashiba (kushoto) wakati wa hafla ya kuzindua tawi jipya la benki hiyo lililopo Sayansi Kijitonyama Dar es Salaam. Katikati ni Mkuu wa kitengo cha Rasilimali Watu, Zainab Mushi.

 

BENKI ya CBA leo imezindua tawi jipya la benki hiyo lililopo Sayansi Kijitonyama jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wateja mbalimbali wa benki hiyo.

 

Katika utoaji huduma za kisasa, Benki ya CBA imepiga hatua kuongeza masaa yake ya kazi ukilinganisha na masaa ya kawaida ya benki kwa tawi lake la Kijitonyama.

 

Kama tawi linalopendwa zaidi na wateja, benki imechukua hatua kuongeza masaa yake ya kazi kutoka saa 2:30 asubuhi hadi 1:00 jioni siku za wiki na hadi 9:00 mchana siku za Jumamosi. CBA pia imeongeza nafasi ya ofisi zake ndani ya tawi hilo ili kupata nafasi kubwa ambayo itawasaidia kuwahudumia wateja wengi Zaidi kwa wakati.

 

 

Mkurugenzi Mkuu wa CBA alisema “Tunaelewa kuna mambo mengi ambayo hutokea wakati wa saa za kazi na kuna baadhi ya wateja ambao wanahitaji kwenda benki lakini wanakosa muda. Kwa hiyo, tumeongeza masaa yetu ya kazi hadi saa 7 jioni ili kuwapa nafasi ya kupata huduma zetu za kibenki katika masaa ziada licha ya muda wa kawaida wa kazi. Pia, tumeongeza nafasi ndani ya tawi letu  ili tuweze kuwahudumia wateja wengi zaidi wanaotembelea tawi letu na pia tumeongeza kitengo cha huduma ya Private Banking kuwapa wateja wetu huduma za kipekee kwenye tawi letu la Kijitonyama.

 

 

Alimalizia akisema, “Kama sehemu ya mipango ya maboresho ya huduma za CBA Bank, hatua hii itaimarisha ahadi ya benki kutoa huduma bora kwa wateja wadogo na wafanyabiashara”.

 

 

Comments are closed.