Dkt. Ndumbaro Akabidhi Zawadi Mchezo wa Gofu wa Mabalozi Zanzibar
BENKI ya NBC imedhamini mashindano ya kwanza ya gofu ya mabalozi visiwani Zanzibar huku ikiahidi kuendelea kusapoti sekta ya michezo na utalii visiwani humo kutokana na mchango wake katika maendeleo ya taifa.
Akizungumza wakati wa mashindano hayo katika Viwanja vya Gofu vya Sea Cliff visiwani humo jana, Mkuu wa Kitengo cha Wateja maalumu binafsi wa Benki ya NBC, Ashura Waziri alisema licha ya kuwa michezo husaidia afya kitu ambacho ni muhimu katika uzalishaji mali, lakini pia michezo yenyewe inaweza kuongeza ajira na kuinua uchumi wa wanamichezo na kwa taifa.
“Naihakikishia Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar kwa kupitia Kamisheni ya Utalii kuwa NBC itaendelea kuisaidia kwenye michezo kama tulivyofanya kwa kudhamini gofu ya mabalozi, tunathamini michezo kwa wafanyakazi wetu pia, tunaihakikishia wizara ya michezo pia tutaendelea kusapoti michezo,” akaongeza.
Naye Meneja wa Tawi la NBC mjini Zanzibar, Ramadhani Lesso alisema NBC imekuwa mdau mkubwa wa maendeleo visiewani humo na ndio sababu ya kuitikia wito wa Wizara ya Habari na Utalii kupitia Kamisheni ya Utalii kushiriki katika mashindano hayo kwani wamekuwa wakishirikia kwa muda mrefu aatika kusapoti utalii visiwani humo.
“Kama mnavyofahamu benki yetu ina ATM zisizopungua 7 hapa Zanzibar na zote zinatoa huduma ya Visa ambayo ni maalumu kwa ajili ya wananchi wote lakini zaidi kwa watalii. Kwahiyo utakuta watalii wanafaidika sana wanapotumia mashine zetu za kutolea pesa na mashine nyingine zilizopo mahotelini.
“Watalii ni muhimu sana kwetu ndio maaana tulipopata mualiko huu kutoka kwa Mkurugenzi wa Kamisheni ya Utalii tuliona ni sehemu muhimu sana kwetu kwa ajili ya kuunga mkono serikali kwa upande wa maendeleo na vilevile ikiwa ni sehemu ya michezo kama ilivyo sera ya michezo,” aliongeza.
Pamoja na hayo meneja huyo akatoa wito kwa serikali na wadau wa michezo kuunga mkono juhudi za kusapoti mchezo wa gofu ufundishwe mashuleni na sehemu zote ili watanzania wote waweze kuucheza a kuupenda.
Katika mashindano hayo, ambayo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Damas Ndumbaro, ambaye pia alikuwa mshiriki, Eliah John aliibuka kidedea kwa kushika nafasi ya kwanza huku Issa Mohamed Chaap wote wa visiwani humo kushika nafasi ya pili.
Comments are closed.