Benki ya Posta yajenga vyoo shule ya msingi Makambi mkoani Ruvuma
Meneja Mwandamizi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Benki ya Posta, Noves Moses akiongea kwenye mkutano katika shule hiyo muda mfupi kabla ya kuzindua vyoo hivyo.
Meneja Mwandamizi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Benki ya Posta, Noves Moses akiwa kwenye picha ya pamoja na walimu wa shule hiyo pamoja na baadhi ya viongozi wa serikali ya mtaa.
|
Akizindua matumizi ya vyoo hivyo vyenye matundu 14, Noves alisema kuwa jamii na taasisi mbalimbali zinatakiwa zitambue kuwa suala la elimu bure linatakiwa liendane na uboreshwaji wa mazingira ya wanafunzi na walimu wawapo shuleni hapo.Alisema kuwa kumekuwepo na baadhi ya wadau wa elimu kulichukulia suala la elimu bure kama kigezo cha kutokuchangia sekta hiyo na baadala yake wanadai ni kazi ya serikali pekee jambo ambalo siyo sahihi katika uboreshaji elimu.
“Suala la elimu bure lisiwe kigezo cha wadau kushindwa kuichangia sekta hiyo kwani kufanya hivyo kunapelekea baadhi ya shule kushindwa kuwa na mazingira mazuri ya watoto kujisomea pamoja na walimu wao kutokuwa na morali ya kufundisha” alisema Meneja mahusiano .
kisasa kwenye shule mbalimbali hapa nchini .