The House of Favourite Newspapers

Benki ya Walimu Waungana na Maxmalipo Kutoa Huduma

Viongozi wa Maxmalipo wakiwa na viongozi wa Benki ya Walimu wakati wa mpango huo wa kushirikiana.

MWALIMU Commercial Bank (MCB) imeongeza matawi ya utoaji wa huduma za kibenki kwa kuwatumia mawakala wa Maxmalipo.

Mfanyakazi wa Maxmalipo akionyesha jinsi kadi za Benki ya Walimu zitakavyokuwa zikitumika kwenye mashine za Maxmalipo.

Hilo limetokana na uzinduzi wa mpango wa benki hiyo wa kuwatumia zaidi ya mawakala 16,000 wa Maxmalipo kutoa huduma zake za kibenki nchini.

Uamuzi huo umefikiwa katika mkutano mkuu wa wanahisa wa benki hiyo unaofanyika  jijini Tanga leo,  Juni 21, 2018.

Mkutano wakati wa uzinduzi wa mpango wa ushirikiano wa Benki ya Walimu na Maxmalipo leo.

Comments are closed.