The House of Favourite Newspapers

Benzema Hakamatiki UEFA, Apeleka Msiba Darajani kwa Mara Nyingine Tena

0
                      Wachezaji wa timu zote mbili wakiwa wamelala chini baada ya mchezo kumalizika

REAL Madrid safari ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa imejibu baada ya ushindi wa jumla ya mabao 5-4 dhidi ya Chelsea.

 

Ni Karim Benzema ambaye alikuwa ni mwiba kwa Chelsea baada ya kupachika bao la ushindi kwa Real Madrid katika muda wa nyongeza.

                                 Karim Benzema akishangilia goli alilofunga dhidi ya Chelsea

Ilikuwa ni Uwanja wa Santiago Bernabeu mbele ya mashabiki 59,839 ubao ulisoma Real Madrid 2-3 Chelsea.

 

Mabao ya Chelsea yalifungwa na Mason Mount dk 15, Antonio Rudiger dk 51 na Timo Werner dk 75.

 

Bao la kwanza kwa Real Madrid lilifungwa na Rodrygo dk 80 ambaye aliweza kuongeza nguvu kwa Real Madrid kusaka ushindi.

 

Thomas Tuchel, Kocha Mkuu wa Chelsea amesema kuwa alikasirishwa na kitendo cha kumuona mwamuzi anacheka na Kocha Mkuu wa Real Madrid Muitaliano Carlo Ancelotti.

 

“Sijapenda kwa kweli kumuona mwamuzi akiwa na muda mzuri na Carlo, (Ancelotti) muda ambao nataka kumwambia asante alikuwa anacheka na kocha wa timu pinzani,”

Leave A Reply