The House of Favourite Newspapers

Betika: Kilichotokea Leo Bunju, Boko na Tegeta, Tazama Mwenyewe

TANGU liingie mtaani takribani mwezi sasa, Gazeti la Betika leo Jumatano, Machi 20, 2019 limweka historia ya aina yake katika mitaa ya Bunju, Boko, Tegeta na viunga vyake jijini Dar es Salaam.

Gazeti la BETIKA ambalo hutolewa bure kwa watu kuanzia miaka 18, liliacha historia kutokana na kugombewa na wasomaji wengi tofauti na mitaa mingine timu ya usambazaji ilipotembelea.

Kama kawaida kila linapoingia mtaani siku ya Jumatano, timu ya maofisa masoko wa Kampuni ya Global Publishers ambayo ndiyo inachapisha gazeti hilo, inaingia mtaani kuligawa gazeti hilo pamoja na kuchukua maoni ya wasomaji.

Leo timu hiyo ilitembelea mitaa hiyo ambapo wasomaji walionekana kuligombania kwa wingi hali ambayo gazeti hilo lilimalizika mapema sana tofauti na siku nyingine.

Jackson Michael ambaye ni mmoja wa wasomaji wa gazeti hilo, alisema kwanza amefurahi kuona amekutana na timu hiyo ya maofisa masoko, lakini fursa aliyopata ya kupiga nalo picha gazeti hilo, ndiyo imemfurahisha zaidi.

“Tangu limeanza kutoka hili gazeti, nilikuwa naenda kuchukua kwenye meza za magazeti kwa sababu huwa naona kwenye matangazo kwamba linatolewa bure na linapatikana kwenye meza za wauza magazeti.

“Licha ya kupata nakala yangu kila linapotoka, lakini kiu yangu kubwa ilikuwa siku moja nipige nalo picha kisha na mimi nitokee kwenye gazeti kama wenzangu. Nashukuru leo ndoto yangu hiyo imetimia.

“Mbali na hilo, pia hili gazeti ni zuri, linatusaidia sana kwa sababu linahusika na masuala ya kubeti, na sisi vijana kwa sasa hiyo ndiyo michezo yetu, hivyo linaturahisishia kushinda mara kwa mara,” alisema Michael.

Naye Ofisa Masoko wa Global Publishers, Mussa Mgema, alizidi kukazia kwamba wamekuwa wakipokea maoni na kuyafanyia kazi juu ya kuliboresha gazeti hilo ambalo hii ni wiki ya sita tangu liingine mtaani ili kuwapatia wasomaji vile vitu wanavyotaka kuvisoma.

“Kila linapokuwa mtaani gazeti hili, tunakutana na wasomaji na kuwaomba kutoa maoni yao ya nini kifanyike kwa ajili ya kuliboresha, kikubwa ni kwamba kila siku tumekuwa tukiliboresha kwa sababu toleo la kwanza haliwezi kufanana na haya matoleo mengine yanayoendelea kutoka kutokana na marekebisho makubwa tunayoyafanya.

“Mbali na maboresho hayo, pia tunawaalika watu mbalimbali kuja kutangaza nasi kwani nafasi za kufanya hivyo zipo wazi, wasisite kuja ofisini kwetu Sinza Mori jijini Dar kwa ajili ya kuleta matangazo yao hayo,” alisema Mgema.

Gazeti hilo lenye kurasa 20 ambazo zote ni za rangi, mbali na kuwa na makala na odds za kampuni mbalimbali, pia kuna takwimu za ligi kubwa barani Ulaya.

PICHA NA DEINIS MTIMA | GLOBAL PUBLISHERS

Comments are closed.