The House of Favourite Newspapers

BETIKA LATIA MAGUU KIBAHA

 


KWA mara ya kwanza, timu ya Maofisa Masoko imewafikia wakazi wa Kibaha mkoani Pwani ambao wengi walikuwa na kiu ya kutoa maoni yao juu ya Gazeti la Betika.

Baada ya timu hiyo kufika maeneo hayo, wasomaji mbalimbali wa Betika walionyesha furaha yao juu ya kuwepo kwa gazeti hilo huku kubwa wakiomba kuongezewa nakala kwani siku zote humalizika mapema na wengine kukosa kopi.

Gazeti hilo ambalo linachapishwa na Kampuni ya Global Publishers, limekuwa likitolewa bure kwa watu wenye umri kuanzia miaka 18 ambapo lina kurasa 20 ambazo zote ni za rangi.

“Tumefurahi sana leo kututembelea huku kwetu, kiukweli ujio wa hili gazeti ni msaada mkubwa kwetu sisi tunaobeti kwani linatusaidia sana.

“Niwapongeze tu wale wote wanaoliandaa, walifikiria sana mpaka kulianzisha kwani huko nyuma hakukuwa na kitu kama hiki hapa nyumbani, wametusaidia sana.

“Mbali na kutusaidia katika kubeti, lakini kuna stori na takwimu mbalimbali za Ulaya ambao zinatufanya tujue mambo mengi kuhusu soka la kimataifa,” alisema mmoja wa wasomaji hao aliyejitambulisha kwa jina la Aman Charles.

Kwa upande wa Ofisa Masoko wa Global Publishers, Mussa Mgema, alisisitiza kwamba, lengo kubwa la Betika ni kumfikia kila Mtanzania katika pande zote za nchi na wao kama timu, watahakikisha wanafika popote pale kwenye makazi ya watu.

“Wasomaji wetu tunawajali sana, kila siku tumekuwa tukiweka vitu vizuri ndani ya gazeti letu hili ambalo huwa tunalitoa bure.

“Tumejipanga kuhakikisha tunafika kila sehemu ambapo kuna makazi ya watu, kubwa zaidi ni kuwafikishia hili gazeti ambalo lina maujanja mengi ya kubeti, hivyo nyie wakazi wa Kibaha endeleeni kulipokea vizuri gazeti letu.

“Pia bado tunapokea matangazo, hivyo hii ni fursa ya watu ambao wanataka kutangaza nasi kuleta matangazo yao kwetu, tunawakaribisha ofisini kwetu Sinza Mori jijini Dar,” alisema Mgema.

Comments are closed.