BETIKA LATUA MIKONONI MWA ZAHERA

 Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera akisalimiana na mhariri wa gazeti la Championi Ijumaa, John Joseph

WAKATI mamilioni ya wanamichezo wenye umri wa miaka 18 na zaidi wakiendelea kuingiza kipato kupitia michezo ya kubahatisha na kutabiri matokeo, wanamichezo wenye wasifu mkubwa nao wamelipokea gazeti hilo vizuri.

 

Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera ni mmoja wa wadau ambao walikabidhiwa gazeti hilo mara baada ya jana kutembelea ofisi za Global Group zilizopo Sinza Mori jijini Dar es Salaam. Kocha huyo raia wa DR Congo, alikabidhiwa gazeti hilo na kuonyesha furaha.

 

Zahera ambaye pia ana uraia wa Ufaransa, alikabidhiwa gazeti hilo na mmoja wa wahariri, John J. Haramba kisha kuuliza juu ya gazeti hilo ambapo alifafanuliwa kuwa ni gazeti la bure na maalum kwa masuala ya matangazo na habari za kimichezo na burudani.

 

Baada ya kukabidhiwa, Zahera alifurahia, akafunua kurasa kadhaa kisha akamkabidhi Ofisa Habari Msaidizi wa Yanga, Godlisten Anderson Chicharito aliyekuwa ameambatana naye. Akizungumzia upande wa gazeti hilo ambalo linaingia mtaani kila Jumatano, Kezilahabi Peresi ambaye ni Ofisa Masoko wa Gazeti la Betika, alisema:

 

“Zaidi ya habari na uchambuzi wa mechi mbalimbali za ligi za nje, gazeti hili litakuwa linakuletea matangazo kutoka katika kampuni zinazoendesha michezo ya kubahatisha. “Betika tunaamini, gazeti letu ni fursa nzuri kwa wabetiji wote kuelewa kwa undani kuhusiana na michezo ya kubahatisha, mambo ya kuzingatia ili kubeti kwa mafanikio na kuvuna fedha kwa wingi,” alisema na kuongeza:

“Kumbuka kuwa ukitangaza na BETIKA utapata ofa ya biashara yako kutangazwa katika channel ya YouTube ya Global TV Online, tovuti ya Global Publishers na kurasa zote za mitandao ya kijamii ya Global Publishers. Unakaribishwa sana BETIKA!

 

“Kwa mawasiliano zaidi fika ofisini kwetu Sinza Mori kwenye Jengo la Global Group mkabala na Wanyama Hoteli jijini Dar es Salaam, au wasiliana nasi kwa namba, 0755-826488, 0712-595636 na 0659-472001 au barua pepe: betika255@gmail.com.”


Loading...

Toa comment