The House of Favourite Newspapers

BETIKA LAZIDI KUTIKISA KITAA

Maofisa usambazaji wa Gazeti la Betika wakiwagawia wasomaji wa gazeti hilo wa eneo la Buguruni Bungoni jijini Dar es Salaam.
Ofisa Masoko wa Global Publishers, Mussa Mgema (kulia) akiwagawia magazeti ya Betika wadau wa gazeti hilo.
Wasomaji wa Gazeti la Betika wakisoma habari mbalimbali zinazopatikana ndani ya gazeti hilo.

 

LIKIWA limetimiza mwezi mmoja tangu liingie mtaani, Gazeti la Betika limezidi kutikisa ambapo kila siku wasomaji wamekuwa wakilimwagia sifa kemkem.

 

 

Gazeti hilo hutolewa bure kwa watu wenye umri kuanzia miaka 18 na huwa linatoka kila Jumatano.

Kila likitoka, maofisa masoko wa Kampuni ya Global Publishers ambayo ndiyo inachapisha gazeti hilo, huingia mtaani kupata maoni ya wasomaji ambapo wengi wameonekana kulimwagia sifa.

 

 

Leo Jumatano, maofisa masoko hao walitinga maeneo ya Msimbazi Center, Ilala hadi Buguruni na kuzungumza na watu kadhaa juu ya gazeti hilo ambalo linahusu zaidi masuala ya kubeti.

“Gazeti hili ni zuri, ukilisoma hata kama hauna mpango wa kubeti basi lazima ubeti kwa sababu linakupa njia nzuri ya kushinda na mara kadhaa watu wanashinda kutokana na mbinu zilizopo humu ndani,” alisema mmoja wa wasomaji.

 

 

Ofisa Masoko wa Global Publishers, Mussa Mgema, alisema kuwa mapokea ya gazeti hilo kila siku yanazidi kuwa juu hali inayodhihirisha kwamba wasomaji hasa wazee wa kubeti walikuwa na kiu kubwa ya bidhaa kama hiyo.

“Gazeti hili ni mahususi kwa ajili ya ishu nzima ya kubeti, lina makala nyingi zinazoelezea kampuni mbalimbali za kubeti, lakini pia humo ndani kuna odds zinazomfanya msomaji kupata njia rahisi za kubeti.

 

 

“Tangu liingie mtaani, tumepata mrejesho mzuri kwamba wasomaji wanalihitaji sana, hivyo tutaendelea kuwapa vitu vizuri wasomaji wetu ili kukata kiu yao.

“Lakini ukiangalia toleo la leo , lina mambo mengi yanayohusu michezo ya kimataifa kama mechi ya Man U na PSG, hivyo watu wa kubeti wanapata maujanja ya kubashiri mchezo huo na kushinda,” alisema Mgema.

 

 

Gazeti hilo lenye kurasa 20 ambazo zote ni za rangi, mbali na kuwa na makala na odds za kampuni mbalimbali, pia kuna takwimu za ligi kubwa barani Ulaya.

Comments are closed.