The House of Favourite Newspapers

Betika linakata mitaa tu

NI siku nyingine tena ambapo gazeti lako pendwa linalotolewa bure la Betika limeingia mtaani ikiwa ni wiki ya 30.

Tangu siku ya kwanza linaingia mtaani, Betika limezidi kuwa gumzo kwa wasomaji mbalimbali ambao wengi wao wamekuwa wakilisifia kila kukicha.

Betika ambalo linachapishwa na Kampuni ya Global Publishers, linatolewa bure kwa watu wenye umri kuanzia miaka 18 na huingia mtaani kila Jumatano.

Gazeti hilo lenye kurasa 20 za rangi linalojihusisha na masuala ya betting na lotto, lina takwimu za ligi tofauti na matangazo mbalimbali ya biashara.

Leo Jumatano, timu ya maofisa masoko ya Global Publishers, ilitembelea Mitaa ya Ilala Boma jijini Dar es Salaam na kukutana na wasomaji mbalimbali wa Gazeti la Betika.

“Uwepo wa gazeti hili ambalo huwa tunalipata bure, kiukweli ni msaada mkubwa kwetu, tunalitumia kujipatia fedha nyingi wakati tunapobeti.

“Mbali na kubeti, niseme tu, Gazeti la Betika ni gazeti ambalo linashika kila kona, ukiachana na watu wa soka, pia hata mama wa nyumbani anaweza kufaidika nalo kwani kuna matangazo ya bidhaa mbalimbali ikiwemo vifaa vya majumbani na mavazi.”

Naye Ofisa Masoko wa Global Publishers, Mussa Mgema, alisema heshima ya Betika imeendelea kukua kila siku na sasa wanajivunia kuwa na idadi kubwa ya makampuni yanayotangaza biashara zao kupitia gazeti hilo hasa kwa kuwa bei yao ni nafuu na imewavutia wengi, huku akiongeza kuwa bado wanawakaribisha watu binafsi na makampuni kuleta matangazo yao.

“Hili ni gazeti la bure, linawahusu watu wazima kuanzia umri wa miaka 18, linatolewa bure kabisa kwa wauza magazeti wote nchini.

“Wote wanaofanya kazi na Betika wanapata ofa ya kutangaziwa biashara zao kwenye mitandao yetu ya kijamii katika Instagram, Facebook, Twitter na Global TV Online.

“Kupitia hayo matangazo ambayo yapo ndani ya Betika, msomaji akijipatia nakala yake anapata faida mara mbili, kwanza kufahamu odds mbalimbali za kubet, lakini pia kufahamu mambo mbalimbali yanayowahusu watangazaji wetu hao.

“Wanaohitaji kutangaza nasi tunapatikana kupitia namba 0755826488 na 0712595636 au barua pepe [email protected], bei zetu ni nafuu, muhusika anaweza kufika Sinza Mori, Dar, kwenye jengo letu la Global Group,” alisema.

Miongoni mwa wasomaji waliokutwa na timu ya maofisa masoko ya Global Publishers, alikuwa Abdallah Ally ambaye alisema: “Gazeti la Betika kila siku limekuwa likiwasaidia watu wengi hasa wale wanaojihusisha na masuala ya kubeti kama mimi.

Comments are closed.