The House of Favourite Newspapers

BI TROPHONIA AIBUKA MSHINDI WA PIKIPIKI KUTOKA TECNO

Ikiwa ni siku ya 15 tangu kuanza kwa shindano la CAMON KAMA ZOTE Kampuni ya simu ya TECNO ilimtaja Bi Trophonia kuwa mshindi wa pikipiki wa shindano hilo la  CAMON KAMA ZOTE katika msimu huu wa kwanza kupitia Lucky draw iliyofanyika katika duka la simu la TECNO lililopo Mlimani City na kurushwa live kuitia  kurasa yao ya @tecnomobiletanzania, ikiwa  imejumuisha maduka yote yenye promotion jijini Dar es Salaam, Mwanza, Tabora, Arusha, Mbeya na Dodoma.

Mshereheshaji wa  hafla hiyo  ambaye ni Ofisa wa digital TECNO, Bi Salma Shafii, katika hafla hiyo  alimkaribisha msanii maarufu wa comed Dully Vanny kuchezesha lucky draw.

 

Baada ya kumalizika kwa burudani kutoka kwa msanii huyo  kampuni hiyo  kuitia Afisa  Masoko wa Kampuni ya simu ya TECNO Bwana Moses Mtweve, ilimtangaza Bi Trophonia kuwa mshindi na  kuahidiwa kupelekewa pikipiki hiyo hadi anapoishi.

Lakini pia haikuishia hapo washindi wengine waliopatikana kupitia kipengele cha maswali na majibu ambao ni Agyprecious Emanuel, Kitongo Nuru, Cluzy Eyes na Ally Famadi ambao wote kwa pamoja  walijishindia stand ya simu, mpira wa TECNO, T-shirt ya TECNO na chupa.

 

 

TECNO inaendelea kuwakumbusha wateja wake kufika kwenye madu yake  na kununua simu za TECNO CAMON Series ili kuingia katika droo ya pili ya pikipiki na zawadi nyingine kemkem.

Kwa habari nyingi zaidi tembelea  http://www.tecno-mobile.com/tz/index.php?id=740#/

Comments are closed.