The House of Favourite Newspapers

Biden Kufanya Mazungumzo na Viongozi wa Afrika Kuanzia Jumanne, Washington DC

0
Rais Joe Biden, wakati huo akiwa makam wa rais, akizungumza wakati wa kongamano la kibiashara kati ya nchi za Afrika na Marekani, mjini Washington DC, Aug 5, 2014

Rais wa Marekani, Joe Biden atakuwa mwenyeji wa viongozi kutoka nchi za Afrika kuanzia kesho Jumanne hapa Washington DC, wakati White House ikiweka mikakati ya kupunguza pengo la ukosefu wa uaminifu kati ya Marekani na Afrika, jambo ambalo limekuwa liokiongezeka kwa muda wa miaka kadhaa.

Utawala wa Biden umepuuza ushawishi wa China na Russia ambao unaendelea kuongezeka barani Afrika lenye takribani zaidi ya watu bilioni 1.3.

Maafisa wa White House badala yake wanazingatia sana namna ya kuboresha ushirikiano wa Marekani na viongozi wa Afrika.

Msemaji wa White House Kaine Jean Pierre, amesema kwamba kongamano la wiki hii ni fursa nzuri ya kuimarisha ushirikiano na bara la Afrika hasa katika biashara, Afya na usalama.

Biden anatarajiwa kutumia fursa ya kongamano hilo la viongozi wa Afrika, kutangaza wanachama wa kudumu wa Afrika katika kundi la nchi 20 zenye nguvu kubwa duniani.

Juhudi za Biden kuimarisha uhusiano kati ya Marekani na mataifa ya Afrika zinajiri wakati ambapo utawala wake umesema kwamba unaamini kuwa ushawishi wa China na Russia barani Afrika unastahili kuzingatia sana maslahi ya Marekani na Afrika.

MR PIMBI AMPIGIA SIMU MKE WAKE ‘LIVE’, UTACHEKA WALICHOKIONGEA – ”MIMI NINA MBAMBAMBA?”…

Leave A Reply