The House of Favourite Newspapers

BIFU LA MAMA MONDI, ZARI SIRI YAFICHUKA!

SIRI ya bifu la mama wa msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Mondi’, Sanura Kassim ‘Sandra’ na ‘mkwewe’ Zarinah Hassan ‘Zari’ imefichuka baada ya mtu wa karibu na familia hiyo kuanika kuwa wawili hao waliingia kwenye mgogoro baada ya mama Mondi kubeba ujauzito. 

 

Sosi huyo alilieleza Gazeti la Amani kuwa, mama Mondi alipata ujauzito na kumueleza mkwewe huyo kuwa anahitaji daktari mzuri kutoka Afrika Kusini ili ahakikishe kuwa ujauzito huo hautoki kwani anahitaji kupata mtoto na mumewe Maisala Shante ‘Anko’ ili aifurahie ndoa yake.

“Unajua kwa nini mama Mondi na Zari waliingia kwenye bifu akamchukia? Ni kwa sababu alimpa siri ambayo alikuwa hajamwambia mtu yeyote ya ujauzito wake yeye akamwambia meneja mmoja wa Diamond ambaye naye alimtania mama bila kujua kuwa ilikuwa ni siri,” alisema sosi.

 

Aidha, sosi huyo alisema kuwa baada ya Zari kumueleza meneja huyo bila kujua kuwa hakutaka mtu ajue na meneja huyo akamtania mama Mondi kuwa ni mama kijacho kitendo ambacho kilimkera ndipo bi’mkubwa huyo alipomchamba Zari. “Unaambiwa mama Mondi alimchamba Zari vibaya na bahati mbaya ujauzito wenyewe ukatoka kwani ulitoka hata kabla hajapata msaada aliokuwa anautaka,” alisema sosi.

Amani ilijiridhisha huenda maelezo hayo ya sosi yana ukweli baada ya kufuatilia ukurasa wa mama Mondi kwa muda wa miezi mitatu na kubaini kuwa mama huyo ameacha ghafla kumposti mkwe wake kwa lolote kitendo ambacho kilizua maneno mengi kwa watu kwani si cha kawaida.Alipotafutwa mama Mondi kuhusu madai hayo, mambo yalikuwa hivi:

 

Amani: Mama kuna ubuyu nimeupata hapa eti uligombana na Zari kisa alikutangazia una ujauzito na baada ya hapo ulitoka je, unaliongeleaje hilo?

Mama Mondi: Sina bifu na Zari mbona huwa nawasiliana naye kwa njia ya WhatsApp na mara ya mwisho amenitumia picha za watoto.

Amani: Mbona haumposti kama zamani na hata ilipofika siku yake ya kuzaliwa hukumposti?

Mama Mondi: Tulishaacha kupostiana siku nyingi ndio maana sijamposti lakini hatuna bifu lolote.

Amani: Je, suala la ujauzito unaliongeleaje?

Mama Mondi: Mbona nilizaa sasa, mtoto ni mkubwa tu.

Amani: Ulizalia wapi mbona hatujasikia na tunawajua Esma na Nasibu tu?

Mama Mondi: Mbona inawezekana tu wewe elewa hivyo na kama huamini ongea na baba (Shamte).

Gazeti hili lilipojaribu kuzungumza na Shamte, alisema yeye hana la kusema. Bifu la mama Mondi na Zari limekuwa likijadiliwa sana mitandaoni huku kila mmoja akianika sababu tofauti za bifu hilo.

Stori: Hamida Hassan na Gladness Mallya

Comments are closed.